Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma
RAIS Samia Suluhu Hassa amesema mwaka huu Tanzania inakwenda kufanya sensa ya makazi ya watu na siyo sensa ya watu pekee yake kama ilivyozoeleka miaka mingine ya sensa.
Aidha amesema,kukamilika kwa mfumo wa anwani za makazi kutarahisisha zoezi la sensa ambalo linatarajiwa kufanyika Ogasti mwaka huu huku akiwataka wahusika wote katika utekelezaji wa mradi wa anuani za makazi wakiwemo wakuu wa mikoa kuhakikisha unakamilika kwa wakati kama ulivyopangwa.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma katika kikao kazi cha wakuu wa mikoa kuhusu mfumo wa anwani za makazi ambapo amesema,mradi huo ni lazima ukamilike mwezi Mei mwaka huu kwani unategemewa katika zoezi la sensa ya watu na makazi .
“Ninyi wakuu wa mikoa ndio mnahusika katika utekelezaji wa mradi huu naomba ukamilike kwa wakati ilituweze kufaniukisha na zoezi letu la sense ambao tunatarajia kulifanya mwaka huu,kwa ambaye atasababisha mradi huu ushindwe kukamilika kwa wakati tutakaa tuongee uso kwa uso .”amesema Rais Samia na kuongeza kuwa
“Kukamilika mwaka huu kutarahisisha mambo mengi ikiwemo zoezi letu la sense ambalo miaka yote kwanza hatukuwa tukipata taarifa sahihi lakini pia kulikuwa na uwezekano wa nyumba nyingine kurukwa,lakini safari hii tutakwenda kuhesabu watu na makazi yote maana mfumo utaonyesha nyumba zote ambazo zitarukwa na hivyo wahusika kurudi kuhesabu tena,”
Aidha amesema katika jutekelezaji wa mradi huo Serikali haitatumia wakandarasi na badala yake watalaam itabidi watumie ubunifu na kuwashirikisha wananchi ili kuokoa fedha nyingi zilizokadiriwa kutumika katika mradi huo.
“Ili kuenda na muda nimeona tuachane na wakandarasi na badala yake tuwatumie wananchi katika kushirikisha kwenye zoezi hili,nilipoletewa bajeti ilinibidi nishangae kwanza kwasababu bajeti ilikuja zaidi ya shilingi Bilioni 700,”amesema na kuongeza kuwa
“Lakini kwa sasa tunapoenda kufanikisha zoezi letu kwa kushirikiana na wananchi gharama zote zimekuwa ni shilingi Bilioni 28 ,hii nikaona inatufaa na tutakwenda na muda sahihi…, nataka hadi kufikia mwezi Mmwaka huu ei zoezi liwe limekamilika,”
Rais Samia amesema kuwa fedha hizo zitagawiwa katika mikoa kulingana na na ukubwa wa mkoa na pia itakuwa ni kwa pande zote mbili za Muungano huku akiwoanya wakuu wa mikoa hao kutumia fedha hizo kwa makusudi yaliyowekwa na siyo vinginevyo.
Kwa upande wake Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah amesema kuwa zoezi la anwani za makazi ni moja kati ya kazi muhimu sana ambapo ikikamilika tanzania itabaki kuwa na historia kwani ni jambo kubwa na lamaendeleo katika nchi.
“Mheshimiwa Rais Nchi inakwenda katika historia hili zoezi ni muhimu na kubwa sana katika Nchi likikamilika litakiwa katika historia,
Naye Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa maagizo waliyopewa na Rais Samia wanayasimamia na kuhakikisha yanatekelezwa kikamilifu ili kufanikisha zoezi la anuani za makazi.
“Nikutoe hofu katika maagizo uliyotupatia tutahakikisha tunayasimamia na kukamilishe mradi huu muhimu kwetu Mimi pamoja na wenzangu hatutakuangusha.”amesisitiza
Mapema,Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema Ukamilishaji huu pamoja na manufaa makubwa yatakayopatikana, utakuwa na tija
katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Mwezi Agosti, 2022.
Amesema,Wizara tayari imejenga uwezo kwa watendaji na wataalamu wa Mikoa na Halmashauri
zote nchini (196 za Tanzania Bara na Zanzibar) kuhusu utekelezaji na Matumizi ya
Programu Tumizi ya Mfumo na kwamba Wataalam hao watawajengea uwezo watendaji wa
Vijiji/Mitaa ambao watatumika katika kukusanya taarifa za anwani za makazi na kutoa anwani husika kwa wananchi.
Kwa mujibu wa Nape mfumo huo ni moja ya hatua muhimu inayokwenda kuijenga Tanzania na kuwa ya kidigitali.
Amesema Mfumo wa Anwani za Makazi ni Muundombinu unaotambulisha
mtu alipo, anapopatikana ama anapotakiwa kuhudumiwa iwe nyumbani, ofisini ama
eneo la biashara. Mfumo wa Anwani za Makazi una tija na manufaa mengi kwa nchi na wananchi wake katika zama hizi za uchumi wa kidijitali.
wa kidijitali nchini.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa