Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Morogoro
NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema kuwa serikali haitavumilia uharibifu wa vyanzo vya maji ambao umekuwa ukifanyika katika maeneo mbali mbali nchini na kwamba serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan imeelekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji na kwamba Wizara haitavumilia uharibifu huo.
Imeelezwa kuwa tayari unaofanywa uchunguzi umeanza kufanyika na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mhandisi Mahundi ametoa onyo hilo katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Morogoro ambapo amesikitishwa na watu wasiojullikana kuharibu miundombinu ya mradi huo unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 3.
Aidha Naibu Waziri huyo ameaonya wananchi wa kijiji cha waliong’oa mabango yaliyowekwa na kuharibu alama za mipaka kwa ajili ya utunzaji wa chanzo cha maji katika vijiji vya Chiwachiwa na Kisegese Wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro.
“Eneo hili la mto Lwipa lipo chini ya usimamizi wa bodi ya maji bonde la mto Rufiji ambao waliweka bikon mia mbili kuzunguka eneo hilo ikiwa ni ishara ya ukomo wa shughuli za kibinadamu lakini kundi la watu wasiofahamika wameng’oa bikoni 180”amesema Mhandisi Mahundi .
Kufuatia uharibifu huo Naibu waziri huyo aliwataka wananchi kuilinda miundo mbinu ya maji kwani serikali inatumia fedha nyingi ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.
Kwa upande wake meneja wa Wakala wa maji vijijini RUWASA Wilaya ya Kilombero ,Flolence Mlelwa amesema kwa sasa serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa tanki la lita laki mbili na nusu na mradi unatarajiwa kuhudumia vijiji vyote Kata ya Mbingu na Igima ambapo vituo thelathini vikitarajiwa kujengwa.
Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godfrey Kunambi ameishukuru serikali kwa kutatua changamoto iliyokuwa inawakabili wananchi wake ya upatikanaji wa maji safi na salama Jimboni kwake.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa