Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Startimes Tanzania wamezindua kampeni maalum ya MARA100ZAIDI ya kampuni ya Star Times kupitia ving’amuzi vyake ambayo imesheheni vipindi na chaneli mbalimbali ndani yake za kuonesha kazi za sanaa, michezo na utamaduni.
Uzinduzi huo umefanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi usiku wa Januari 6, 2022 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Akizungumza kwa niaba ya Wizara na Serikali kwa ujumla katika uzinduzi huo Dkt. Abbasi amewapongeza Star Times kwa kuazisha chaneli mpya maalum kwa ajili ya kuonesha maudhui kutoka Tanzania pekee iitwayo ST Bongo.
Amesema mwaka huu 2022 Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na Wizara wamejipanga kufanya mambo mengi makubwa ikiwemo kutoa mirabaha kwa wasanii, kuimarisha Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni na kuwataka wadau kutimiza wajibu wao.
Ameongeza kuwa wadau wa sanaa hatuna budi kumuombea Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan dua njema kwani ametenda makubwa kazika sanaa na michezo mwaka 2021 ili azidi kuwatendea mema zaidi Watanzania na mengi zaidi katika tasnia za ubunifu na burudani.
Naye Mkurugenzi wa masoko na mahudhui kutoka Startimes Tanzania, David Malisa amesema vitu vilivyopo katika king’amuzi cha startimes atajipatia vitu vingi kwasababu starTimes ni kisimbuzi cha wananchi na kwa mwaka huu wameamua kuja na kitu kikubwa kitakachowawezesha wananchi kuburudika, kufurahika na kwa bei nafuu.
Aidha Malisa amesema kuhusu bei ya kwenye king’amuzi na vifurushi vyake ni rahisi na unaweza kulipia hadi kwa siku;
“Startimes Tanzania ni kampuni pekee ambayo unaweza ukalipia kwa siku, wiki na mwezi, yote hiyo ni kitu kikubwa sana hivyo kwa msimu huu watazamaji wote wasiwe na wasiwasi kwasababu tumewaletea vitu vikubwa zaidi”
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili