November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa inaendelea kuongezeka kufikia nyuzijoto 1.5.

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),imesema wastani wa ongezeko la joto Duniani unatarajia kufikia nyuzi joto 1.5 kati ya mwaka 2030 na 2052 endapo kasi ya  mabadiliko itaendelea kwa viwango vya sasa.

Hayo yameelezwa jijini hapa leo na  Mtafiti kutoka Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania(TMA),Dkt Ladislaus Chang’a wakati akiwasilisha matokeo ya utafiti kuhusu mabadiliko ya hali hewa Tanzania,hali halisi na inavyotarajiwa katika miaka 100 ijayo yaliyokwenda sambamba utoaji wa mihtasari ya vijarida sera vya sayansi na teknolojia vya sekta nne za Afya,kilimo,Maliasili na utalii ulioandaliwa na Tume ya taifa ya sayansi na Teknolojia[COSTECH].

Amesema, kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa Duniani kote inaendelea kuongezeka kila mwaka na athari zake katika sekta zote za kiuchumi na kijamii zinaendelea  kuwa kubwa hususan kwa nchi zinazoendelea ambazo uwezo wake wa kuhimili na kukabiliana na athari hizo ni mdogo.

Akieleza tathmini za kisayansi za mabadiliko ya hali ya hewa Tanzania Dkt.Chang’a amesema zimeendelea kufanywa na wataaalam mbalimbali hapa nchini ikiwemo mamlaka ya hali ya hewa  zinaonesha mwelekeo wa kuongezeka kwa kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake katika sekta zote za kiuchumi na kijamii.

Amesema,mabadiliko haya hujidhihirishwa na kuongezeka kwa joto katika mikoa yote hapa nchini ambapo joto la juuna joto la chini vimeendelea kuongezeka  huku joto la chini likiongezeka kwa kasi zaidi .

“Tathmini zinaonesha kuwa matukio ya vipindi vya hali ya hewa ikiwemo matukio ya ukame ,mafuriko na vipindi vifupi vya mvua kubwa na upepo mkali vimeendelea  kuongezeka katika maeneo mbalimbali na kusababisha athari kubwa kiuchumi na kijamii,”amesema.

Awali akifungua hafla hiyo iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi ,Teknlojia na Ubunifu (COASTECH) mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa COASTECH Dkt.Wilbert  Manyilizu alisema, lengo la warsha  hiyo ni kuwashirikisha Wadau wakuu wa matokeo ya tafiti za kisayansi na  Teknolojia ili waweze kuwasilisha na kutoa matokeo ya tafiti zao.

                                           Amesema,Coastech iliwaita watafiti katika Sekta nne za awali ambazo ni sekta ya Afya,Kilimo,maliasili na mifugo  ili wawasilishe tafiti zao ambazo hufanyiwa kazi na Tume hiyo ambayo ndio yenye dhamana ya kuishauri Serikali katika masuala ya sayansi na teknolojia.


Aidha amesema,lengo la kuanzishwa kwa Tume hiyo ni  kuishauri Serikali katika masuala ya sayanasi na Teknolojia na ubunifu huku akisema,jukumu kubwa la COASTECH ni kuratibu na kuhamasisha Mambo ya utafiti na ubunifu ambapo katika jukumu hilo pia kuna majukumu mengine.

Ameyataja majukumu hayo kuwa ni pamoja na kusimamaia Menejimenti ya maarifa yanayopatikana katika ubunifu na utafiti na baadae kusambaza kwa Wadau huku akisema, michakato yote ya kuwatambua na kuwawezeaha wabunifu ni jukumu lao.

Amesema jukumu linguine la Tume hiyo ni kuhabarisha Wanachi na Wadau mbalimbali kwa kukusanya na kusambaza taarifa za sayansi  na ubunifu wa wananchi pamoja na kusambaza vijarida