Na Cresensia Kapinga, TimesMajira,Online Songea.
WANANCHI wa Manispaa ya Songea wamepongeza Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARULA) kwa kujenga barabara kwa kiwango cha rami na kuweka taa, hatua ambayo itapunguza uharifu katika maeneo hayo.
Wakizungumza na nyakati tofauti jana, mjini hapa Ramadhani Nyoni, amesema wamezoea kuona rami zinawekwa kwenye kata zilizopo katikati ya mji, lakini TARURA wameamua kujenga barabarani hizo pembezoni mwa mji, jambo ambalo huko nyuma lilikuwa halijazoeleka.
Eligia Kapinga mkazi wa Kata ya Msamala amesema kutokana na TARURA kuzipa umuhimu barabara za pembezoni kwa kuzijenga kwa kiwango cha rami, wana imani kubwa kwa kata zao zitafikiwa na miradi ya aina hiyo.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Wilaya ya Songea, John Ambrose amesema kuwa barabara hizo zenye urefu wa kilomita 1.5 zimejengwa kwa gharama ya sh. milioni 900 sambamba na uwekaji wa taa pamoja na mitaro.
Alisema barabara hizo zimejengwa chini ya mkandarasi, Liyuku Matembo ambaye ameshakamilisha uwekaji wa rami kilichobaki kwa sasa ni kazi ndogo ndogo za ufungaji wa taa pamoja na kumalizia mitaro katika baadhi ya maeneo.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu