November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM Mkoa wa Lindi wapata pigo

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

CHAMA cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kilwa ,kata ya Njinjo, Kijiji cha Njinjo mkoani Lindi kimepata pigo baada ya wananchama zaidi ya 200 kurudisha Kati zao Kwa katibu wa tawi la Mkunguni kijijini hapo Mohamed Kazembe Kwa kile walichodai kuwa viongozi wa serikali na Chama ngazi ya wilaya kushindwa kuwasikiliza madai yao.

Wanachama hao wamesema kuwa wamelazimika kurejesha kadi hizo hadi pale ufumbuzi wa ujenzi wa kituo cha afya kata ya Njinjo utakapopatikana kinyume na hapo basi hawaoni haja ya kumwanachama wa chama hicho ambapo kwenye kero badala ya kutatua ndio anakuza.

Akizungumza mara baada ya kupokea kadi hizo huku waandishi wa habari wakishuhudia katibu huyo wa tawi Kazembe Amesema hana chakufanya kwani wanachama hao wamerudisha kadi kutokana na hasira ya kukosa kituo cha Afya Njinjo na mbaya zaidi Rais Samia Hassan alishatoa sh milion 250.

” Kwa hali hii ndugu wanahabari mimi nafanyaje na wameshaamua .kimsingi viongozi wetu wa serikali ngazi ya wilaya wamekosea sana haiwezi maamuzi ya ujenzi wa kituo cha afya Njinjo ubatilishwe ghafla tena pasipo kujulishwa wananchi. Amesema

Kazembe Amesema ni pigo kubwa sana kuona wanachama hawa wanaondoka tena kwasababu ya jambo ambalo liko wazi na fedha yake rais ameshatoa fedha hizo ambazo ni sh.milioni 250

Akizungumzia mvutano huo kati ya serikali ngazi ya wilaya na wanakijiji Katibu wa CCM wilaya Mayasa Kimbau Alisema yeye kama katibu amesikia taarifa za Njinjo kwamba wanachama wamerudisha kadi hizo lakini anasubiri taarifa rasmi kutoka huko.

Amesema kijiji hicho kinawanaccm wengi mno na huko ya nyuma Njinjo ilikuwa chini ya upinzani hivyo lazima wafike huko ili kukutana na wananchi na kulizumgumzia sakata hilo ili mambo memgine yaendelee.

” Tutakwenda Njinjo tunasubiri hasira zao zipoe ili tukasikilizane vizuri lakini pia niwaomba kwamba wawe watulivu kwani hakuna sababu ya kuvurugana sisi sote wanaccm .”amesema katibu Mayasa

Katibu huyo Aliongeza kuwa wao Kama chama kazi yao nikupokea taarifa za kusimamia yale ambayo serikali wanafanya na si vinginevyo hivyo kuhusu kata ya Njinjo na kinachodaiwa kufanyika watakwenda huko kuzungumza na wanaccma na wanachama na anaamini watakwenda kuelewana tu

“unajua mambo mengine ni yakuzungumza na kuelewana kwani hata hiki kinachoendelea ni wananchi kueleweshwa tu hawa watu wote ni wamoja wala hakuna shida au tatizo. “amesema Mayasa

Wananchi wa kata ya njinjo kijiji cha Njinjo kwa muda sasa wapo katika msuguano juu ya wapi kituo cha afya kitajengwa huku wananchi hao wakishinikizwa kituo kijengwe kijiji cha Njinjo kwani ndio katikatika ya vijiji vyote vitatu lakini ndio makao makuu ya Tarafa ya Njinjo.

Katibu wa CCM tawi la Mkunguni Njinjo wilayani kilwa Mohamed Kazembe akizungumza mbele ya wananchi kuhusu kupokea kadi za wanachama wa CCM.