November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi wa Njinjo wamlilia rais Samia ujenzi wa kituo cha afya

Na David John Njinjo timesmajiraonline

WANANCHI wa Kijiji Cha Njinjo Kata ya Njinjo Tarafa ya Njinjo wilaya kilwa mkoani Lindi wamemuomba rais Samia Suluhu Hassan kuingilia Kati mgogoro uliopo kati yao na uongozi wa serikali wilayani humo wa kutengeua maamuzi ya rais ya kujenga kutuo cha afya njinjo na badala yake kuelekeza ujenzi huo kipindimbi.

Wananchi hao wamesema kuwa rais Samia katika juhudi zake za kuimarisha afya za wananchi wake na katika kijiji hicho ambacho kinabeba kata alipeleka shilingi milioni 250 lakini cha kusikitisha viongozi wao wanahamisha kituo hicho na kupeleka kijiji cha kipindimbi.

Akizungumza mbele ya wananchi wake katika mkutano ambao umefanyika kwenye eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Njinjo Muhidin Omar Amesema kuwa kumsingi wamesikitishwa sana juu ya maamuzi ya viongozi wao ngazi ya wilaya.

“katika hili mimi Kama kiongozi nimefika hadi Dodoma kwa lengo la kuonana na katibu Mkuu wa chama. Lakini tumhoji sana juu ya maamuzi haya ambayo yamefanyika haiwezi fedha umeletwa kwa ajili ya njinjo alafu watu kwa utashi wao wanapeleka kungine'”Amesema Omar

Amesema kuwa yeye Kama kiongozi anasimama na wananchi wake katika kile ambacho wanakidai na wanamuomba rais Samia kuingilia Kati sakata hilo ambalo linasababisha hasira kubwa dhidi ya wananchi na serikali yao.

Mwenyekiti Omar Amesema Rais Samia ametoa sh.milioni 250 kwa ajili ya kituo cha afya kijiji cha njinjo ambacho pia ndio kimebeba jina la kata hiyo nakwamba uongozi wao ngazi ya wilaya uliwahamasisha wananchi hao kusafisha eneo la ujenzi wa kituo jambo ambalo wao wamelifanya ikiwa pamoja na kufyeka njia ghafla leo wanasema kituo kiende kipindimbi.

Naye Tabia Mahamud kiloboto ambaye aliwahi kuwa diwani viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi CCM Amesema maamuzi ya viongozi wao hao ni ya kushangaza Sana na yamesababisha maumivu makali kwa wananchi. haiwezikani fedha zimepelekwa kwa ajili ya kituo cha afya njinjo alafu wengine wanahamisha kupeleka kungine.

“Hatutakubali na tunamuomba rais Samia ajuwe Njinjo kuna shida kubwa wananchi tunayumbishwa Sana. Tunamuomba aingilie kati suala hili kwani sisi tumetoa nguvu zetu kwa ajili ya kuandaa Mahala pakujenga kituo cha afya alafu watu wachache kwa maslahi yao wananyanyasa wananchi. “Amesema

“Njinjo mbali yakuwa ni kata lakini pia ndio makao makuu ya tarafa na kituo kilijengwa hapo kwasababu ni katikatika ya vijiji vyote tisa ambavyo vipo ndani ya Tarafa hii ikiwamo kijiji cha Njinjo. “Amesema mmoja wa viongozi waliowahai kupita wilayani humo.

Amesema kuwa watu wanachanganya Sana kimsingi wananchi wa kijiji cha njinjo wanamadai ya msingi sana kwani kituo hicho kilijengwa hapo sababu ni katikati ya vijiji vyote hivyo kitendo cha kuhamasha ni kwenda kinyume na maamuzi ya awali.