Na Esther Macha,Timesmajira,Online,Mbeya
WANANDOA wameshauriwa kuandika wosia katika familia zao ili kujiepusha na migogoro pindi mmoja kati ya wanandoa anapotangulia mbele za haki.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Usajili Msaidizi wa Vizazi na Vifo (RITA), Joseph Mwakatobe wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria ambayo inafanyika kitaifa mkoani mbeya katika uwanja wa Ruanda Nzovwe jijini Mbeya.
Amesema miongoni mwa mambo yanayosababisha migogoro kwa familia ni kutokuwepo kwa wosia ambapo wakati wa mganwanyo wa mali kunaibuka malumbano ambayo yanasababisha chuki.
Amesisitiza ni muhimu kila wanandoa kuzingatia kuandika wosia wanagali hai ili kusaidia kizazi kinachobakia kuishi kwa amani na utulivu.
“Rita ikiwa kama chombo cha serikali inateuliwa kusimamia mirathi yenye migogoro ,lakini changamoto nyingine ya watanzania walio wengi hawaandki wosia na kudhani kuwa wakiandika wosia ni kujichuria kifo ,unapoondoka unaacha familia yako vipi hivyo Rita inahamasisha watanzania namna gani.nzuri ya kuandika wosia na namna ya kuhifadhi “amesema.
Hata hivyo amesema kuwa ili kuilinda familia yako ni vema kuandika wosia ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima kwa ndugu pmoja na kuepuka mateso kwa mke na watoto.
Aidha amefafanua kwamba majukumu ya Rita ni inaandikisha na kuhifadhi wosia hilo ni lengo ambalo limekuwa likisisitizwa hasa kwa wananchi ili kuepukana na migogoro inayotokana usimamizi wa mirathi.
“Mirathi mingi inapata changamoto namna ya usimamizi wa mirathi kutokana na kwamba ndugu kutoelewana au utakuta familia nyingine zinakuwa tofauti na kuleta mgogoro kutokana na kuwa na wake wengi”amesema Mwakatobe.
Mkuu  wa Mkoa wa Mbeya ,Juma Homera amefurahishwa na huduma zinazotolewa na RITA na kuwaomba kuendelea kutoa elimu ya umuhimu wa kuandika wosia ambayo inaweza kupunguza migogoro na vurugu kwenye familia.
Alisema ili kutokomeza wimbi la mauaji kuandika wosia kunaweza kuwa mwarobaini wa kushughulia tatizo hilo kwani kila mmoja atafanya kazi kwa bidii ili kumiliki uchumi wake.
“Ndugu mnaohusika na Rita toeni elimu kwa wananchi wasaidieni namna ya kuandika wosia na kuhifadhi hii itasaidia namna bora ya kuepuka migogoro ambayo imekuwa ikitokea katika jamii ,na nyie wananchi msiogope kuandika wosia kwa kuona mnajichulia vifo amesema Homera.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi