November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naibu Spika Tulia azifunda taasisi za fedha utoaji mikopo kwa wanawake

Na Esther Macha ,Timesmajira,Online,Mbeya

NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson, amezitaka taasisi za fedha hasa Benki ya Biashara ya Tanzania (TCB)  kutowakopesha wanawake mikopo kabla ya kufanya tathimini ya miradi walioanzisha ili kukwepa changamoto ya marejesho kwa wakati

Dkt. Tulia amesema hayo jana wakati wa uzinduzi wa kongamano la wanawake wa Mkoa wa Mbeya lililoandaliwa na TCB kwa lengo la kuwainua wanawake kiuchumi.

Amesema kumekuwa na changamoto ya mali na za wananchi kupigww mnada  kutokana na kukwama marejesho

“Uwezo huo mnao niwaombe msaidie wanawake hawa katika lile lengo lenu la wanawake kuwakuza kiuchumi msipofanya hivyo mtafanya wanawake wawe maskini,” amesema Dkt.Tulia.

Hata hivyo amesema uwezo huo wanao wa kuhakikisha wanawake wanasonga mbele na kuunga juhudi za Rais Samia Suluhu za kuwainua wanawake na kuwaletea maendeleo Watanzania.

Aidha Dkt .Tulia amewataka wanawake kujifunza na kupanua uelewa wao pamoja na kuwa wabunifu kwa kuvuka hatua nyingine ya kimaendeleo. “Lazima wanawake muwe watu wa kujiongeza lakini kujiongeza ndio huu mkopo sasa usikope wakati hujawaza hapo pakubwa pa kutaka kuongeza hiyo biashara yako.”amesema.

Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, akikagua baadhi ya biashara za wanawake wanazozalisha

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Rashid Chuachua amesema wanawake wana changamoto nyingi zipo ambazo zipo ndani ya mfumo, nyingine zimerasishwa sababu zipo ndani ya sheria ukiangalia sheria ya kimila ya mwaka 1963 na zingine za ndoa.

Ofisa Mtedaji Mkuu wa TCB, Sabasaba Moshingi amesema benki hiyo ina wateja. milioni1 na kwamba kati yao asilimia 50 ni wanawake wanafanya vizuri biashara zao.

“Ndugu mgeni rasmi wana hisa wa benki hii asilimia 83 inamilikiwa  na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Shirika la Posta la Simu hii ni benki ya umma inayomilikiwa na serikali,”amesema Moshingi.