Na Mwandishi Wetu
Rais Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua Tamasha la Kwanza la Michezo la Wanawake la Tanzanite litakalofanyika katika viwanja vya Uhuru na Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kuanzia Septemba 16 hadi 18, 2021 huku uzinduzi rasmi ukifanyika Jumamosi, Septemba 18.
Katibu Mkuu anayesimamia sekta za Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt.Hassan Abbasi, ameyasema hayo leo Septemba 15, 2021 alipozungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
“Toka aingie madarakani Rais Samia ameonesha nia ya dhati ya kuinua michezo kwa wanawake hivyo amekubali kuja kuzindua Tamasha hili ambalo litaanza tarehe 16-18 Septemba, 2021’” Amefafanua Dkt. Abbasi.
Amesema Tamasha hilo la kihistoria limesheheni michezo mbalimbali ikiwemo Riadha, ndondi, soka, netiboli, mpira wa kikapu, wavu, karate, Makomando wa kike, kuvuta kamba, rede na mingine mingi.
“Katika kunogesha Tamasha hilo kutakuwepo wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya huku asilimia zaidi ya 98 wakiwa ni wakike ambao nao wataonesha uwezo wao,” amesema Dkt. Abbasi.
More Stories
Walimu elimu ya lazima watatakiwa kuwa wabobezi kwenye masomo wanayofundisha
Wahakikishiwa usalama siku ya kupiga kura
CCM inabebwa na kazi nzuri za Rais Dkt. Samia-Makalla