November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chuo Kikuu Mzumbe watambulisha mradi wa mageuzi sekta ya elimu

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online,Morogoro

MENEJIMENTI ya Chuo Kikuu Mzumbe imeutambulisha mradi wa mageuzi ya sekta ya elimu kwa ajili ya kuchochea uchumi ‘Higher Education for Economic Transformation – HEET’ wenye lengo la kuongeza udahili kwa kujenga miundombinu na kuboresha mitaala ili kuendana na soko la ajira la sasa.

Prof.Lughano Kusiluka akifungua kikao cha Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe kilichofanyika katika ukumbi wa Samora

Akizungumza katika kikao na Wafanyakazi wa Kampas kuu Morogoro, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof.Lughano Kusiluka, amesema ni vyema Watumishi kujiandaa na kuchangamkia fursa zilizopo katika mradi huo mkubwa wa miaka mitano ambao utahusisha ujenzi wa miundombinu na kuwaendeleza Watumishi kitaaluma.

“Ifikapo mwaka 2025 majengo yanapaswa kuonekana na hivyo tunapaswa kuwa na kasi kubwa ya utekelezaji wa mradi huo” amesisitiza Prof.Kusiluka.

Wafanyakazi wa Kampas kuu wakisikiliza hotuba ya Makamu Mkuu wa chuo katika kikao kilichofanyika hivi karibuni

Awali akitoa taarifa kuhusu mradi huo Mratibu msaidizi wa mradi huo,Dkt.Hawa Tundui, amesema Chuo kikuu Mzumbe kimetengewa Dola Milioni 22, kwa ajili ya kutekeleza mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, ambapo asilimia 80 ya fedha hizo ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na 20 ni kwa ajili kuwaendeleza Watumishi kitaaluma na kutengeneza mitaala mipya ya elimu.

 Mratibu wa mradi Dkt. Hawa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ‘HEET’ katika kikao cha Wafanyakazi
aibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe anayeshughulikia, Prof.William  Mwegoha akizungumza na  Wafanyakazi
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe anayeshughulikia Utawala na Fedha, Prof. Allen Mushi,  akizungumza na  Wafanyakazi
Wafanyakazi wakifuatilia hotuba za Viongozi katika kikao cha Wafanyakazi
……