Na Joyce Kasiki, TimesMajira,Online,Dodoma
MBUNGE wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima, leo amefika mbele ya Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, kwa ajili ya kuhojiwa kuhusiana na tuhuma zinazomkabili, huku akikataa kukalia kiti alichokuwa ameandaliwa.
Mbali na kukataa kiti alichokuwa ameandaliwa, pia Askofu Gwajima alikataa kutumia kipaza sauti alichokuwa ameandaliwa na badala yake kuomba apatiwe kingine.
Askofu Gwajima amefika mbele ya Kamati hiyo jijini Dodoma leo, ambapo baada ya kukataa kukalia kiti na kipaza sauti alichokuwa ameandaliwa, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka, alimsihi kukalia kiti alichoandaliwa pamoja na kisaza sauti kwamba havina shida yoyote, lakini alishikilia msimamo wake.
Wakati anakataa kukalia kiti alichokuwa ameandaliwa tayari Askofu Gwajima alikuwa ameshikilia kiti kingine kilichokuwa pembeni, hivyo wakati Mwenyekiti wa Kamati, Mwakasaka akielekeza apewe kiti kingine, yeye alivuta kiti hicho na kukikalia.
Aidha, Mwakasaka alikubali ombi la Askofu Gwajima la kutaka abadilishiwe kipaza sauti.
Awali baada ya Askofu Gwajima kufika Bungeni leo mchana, wajumbe wa Kamati hiyo walilazimika kumsubiri kwa takiribani dakika tatu kwa maelezo kwamba amemtuma msaidizi wake akamchukulie dawa zake kwenye gari yake, ndipo afike mbele ya Kamati.
Mwenyekiti wa Kamati aliwaambia wajumbe wa Kamati kwamba hakuwa amejua kama Askofu Gwajima ana tatizo lolote la kiafya. Baada ya hapo ndipo alipoingia kwenye ukumbi uliandaliwa kwa ajili ya mahojiano na kutoa masharti ya kukataa kiti na kipaza sauti.
Askofu Gwajima, juzi alikiri kupokea barua ya wito wa kuitwa kwenye Kamati hiyo. Askofu Gwajima alithibitisha kupokea barua ya wito wa kuitwa kwenye Kamati ya Haki wakati akizungumza na waumini wake jana kanisani.
“Nimepokea barua ya Spika kwenda kwenye Kamati, nitakwenda. Nimesema hapa
kwa kuwa aliyenitumia barua ameweka mitandaoni akisema kwanini nimesema hapa na yeye aniambie kwa nini aliweka mitandaoni,” alisisitiza Askofu a Gwajima.
More Stories
Rais Samia afanya uteuzi
Waliombaka, kulawiti binti wa Yombo, Dar jela maisha
BREAKING NEWS: Rais Dkt Samia afanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali usiku huu