Na Mwandishi wetu,Timesmajira,Online
CHAMA Cha Mapinduzi CCM, kimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mkoani Shinyanga ambaye pia Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Elias John Kwandikwa kilichotokea Agosti,2 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiendelea kupatiwa matibabu.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi,Shaka Hamdu Shaka kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Samia Suluhu Hassan amesema Chama kimepoteza mtu muhimu aliyekuwa na mchango mkubwa kwa CCM na Utumishi wa Umma.
Amesema wamepoteza mwanachama wa CCM na mtu muhimu ambaye mchango wake katika utumishi wa umma hautosahaulika.
“Alikuwa ni kiongozi shupavu na makini aliyetekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria na Utaratibu,”amesema Samia Suluhu Hassan
Amesema Elias John Kwandikwa, amekuwa Mjumbe wa kamati ya siasa katika wilaya za Kibaha Mjini 2012-2015, Kahama 2015 mpaka sasa na Mjumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga 2015 na Mbunge wa jimbo la Ushetu toka 2015-2021.
Aidha amesema kuwa Naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mwaka 2017-2020 na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa hadi umauti unamfika.
“Chama Cha Mapinduzi(CCM) kinatoa pole na kuwaombea subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa mpendwa wao familia ya marehemu, wananchi wa Jimbo la Ushetu, Ndugu, Jamaa, Marafiki na wote walioguswa na msiba huu,”amesema
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti