January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ziara ya kwanza ya Mkuu wa Chuo Kikuu Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU) Anne Makinda chuoni hapo

Mkuu wa chuo cha Hubert Kairuki (HKMU), Anne Makinda akipata maelezo kutoka kwa Muuguzi wa shule ya Uuguzi ya Hubert Kairuki alipotembelea chuo hicho kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo hivi katibuni
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Profesa Charles Mgone akimweleza jambo Mkuu wa Chuo hicho, Anne Makinda kuhusu ujenzi wa kampasi mpya ya chuo hicho iliyopo Boko wakati alipotembelea chuo hicho kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika wadhifa huo hivi karibuni. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, John Ulanga na Mwenyekiti wa Bodi ya KHEN, Kokushubira Kairuki.
Mtaalamu wa maabara wa Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki (HKMU), Walter Msangi akimweleza Mkuu wa Chuo hicho, Anne Makinda kuhusu shughuli zinazofanywa na maabara hiyo katika kufundisha wanafunzi wa chuo hicho wakati wa ziara yake chuoni hapo jana. Anayefuata ni Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Charles Mgone, Makamu Mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia taaaluma Profesa Moshi Ntabaye na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, John Ulanga
Makamu Mkuu wa chuo cha Hubert Kairuki (HKMU), Profesa Charles Mgone akimweleza jambo Mkuu wa chuo hicho, Anne Makinda alipotembelea chuo hicho jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, John Ulanga na kushoto ni Makamu Mkuu wa HKMU anayeshughulikia taaluma Profesa Moshi Nyabaye.
Mkuu wa chuo cha Hubert Kairuki (HKMU), Anne Makinda akielekea kwenye famasi iliyoko hospitali ya Kairuki kwenye ziara yake aliyoifanya jana kwenye vitengo mbalimbali vya chuo cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, John Ulanga.