Na Bakari Lulela, TimesMajira Online, Dar
JESHI la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala limewataka wananchi eneo hilo wanaotumia nishati ya gesi kwa matumizi ya nyumbani kuwa makini na vihatarishi vinavyosababisha milipuko ya moto.
Akizungumza Dar es Salaam Mratibu Msaidizi wa Jeshi la zimamoto Mkoa wa Ilala Elisa Mugisha amesema matumizi ya nishati ya gesi kwa sasa yamekuwa yakiongezeka hali inayopelekea watumiaji na uelewa katika kuhifadhi kwenye mazingira salama yasiyo kuwa na joto.
“Gesi ni nishati muhimu kwa matumizi ya majumbani ambapo ikitumika vibaya inaweza kusababisha milipuko ya moto na kuleta taharuki kubwa ndani ya jamii,” amesema Mratibu Msaidizi wa jeshi hilo.
Aidha Mratibu huyo ameeleza kwamba wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari ya utumiaji sahihi wa bidhaa hiyo ambapo mtungi wenye gesi unatakiwa kuhifadhiwa nje ya nyumba huku mpira utumike kupeleka gesi eneo husika (jikoni).
Hata hivyo Mkuu huyo ameeleza unapokuwa unatumia gesi ni vema kuepuka vihatarishi, joto kali na umakini na uvujaji wa gesi unaotokana na kuchubuka kwa mpira unaosafirisha kutoka kwenye la mtungi kwenda eneo husika ambao unaweza kusababisha kutokea kwa mlipuko mkubwa wa moto.
Katika hatua za usafirishaji wa bidhaa ya gesi Mratibu Mugisha amesema kwa usalama nishati ya gesi inatakiwa kutumia usafiri wake ambapo haifai kuwekwa katika magari ya abiria kwa kuwa bidhaa hiyo inaweza kulipuka na kuhatarisha usalama wao na mali zao.
Wito umetolewa na Jeshi la Zimamoto na uokoaji kuwa wanaotumia nishati hiyo kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani wahakikishe wanapata uelewa kuhusiana na matumizi sahihi ya bidhaa ya gesi ili kujiweka katika mazingira salama, kama kutatokea mlipuko utakao sababisha janga la moto pinga namba 114 kwa kupatiwa huduma na kikosi cha zimamoto na uokoaji.
More Stories
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar
CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo
Walimu elimu ya lazima watatakiwa kuwa wabobezi kwenye masomo wanayofundisha