November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Stanbic yazindua kampeni maalumu ya madawati

Na Bakari Lulela,TimesMajira Online

BENKI ya Stanbic imezindua kampeni maalumu ya Stanbic madawati initiative yenye lengo la kuendeleza na kuinua sekta ya elimu nchini ambapo imeikabidhi serikali jumla ya madawati yapatayo 2000.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi, Joyce Ndalichako (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya stanbic madawati intiative iliandaliwa na Stanbic benki Dar es Salaam kulia kwake ni afisa mkuu masoko wa benki hiyo Desideri Mwegelo,kushoto ni mkuu wa kitengo cha biashara Omari Ntiga.

Akizungumza Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi,Prof. Joyce Ndalichako ameipongeza benki hiyo kwa kuonyesha uzalendo wa kweli wa kuwekeza kwa minajili ya kuwasaidia Watanzania kupata elimu bora.

“Serikali inatambua mchango wenu hivyo tunawapongeza kwa kuanzisha kampeni hii ya Stanbic madawati initiatives yenye lengo la kuisaida jamii katika upatikanaji wa elimu bora shuleni,” amesema Prof.Ndalichako

Prof. Ndalichako ameeleza kuwa pamoja na uzinduaji wa kampeni hiyo Stanbic benki imekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi ambapo ameweza kuchangia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuisaidia jamii.

Hata hivyo Waziri huyo amesema kwamba elimu ni mhimili mkubwa katika maisha ya mwanadamu hivyo faifa lolote haliwezi kupata maendeleo katika uwekezaji bila ya kuwa na elimu.

Aidha Profesa Ndalichako amesema kwamba ndoto za maendeleo zitafanikiwa kama kutakuwa na ushirikiano mzuri baina yetu na elimu ndio msingi wa maisha hivyo ni vema kuhakikisha vijana wetu wanaipata.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo Omari Ntiga amesema benki yao imekuwa ikishiriki katika mipango mbalimbali ya kuisaidia jamii hususan katika sekta ya elimu, kilimo pamoja na utoaji wa huduma za bima za afya kwa wananchi.

Hata hivyo benki ya Stanbic imekuwa na utaratibu wa kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania wanaokuwa wakihitimu kutoka vyuo vikuu.