Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online
BODI ya Korosho imesema ina mpango wa kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa tani 300,000 hadi kufikia wastani wa tani 700,000 ifikapo mwaka 2025/26.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Francis Alfred ameyasema hayo katika maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Saam (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar huku yakitarajiwa kufuguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Leo.
“Wakati tukifikiria kwenda kuongeza uzalishaji wa korosho ghafi, tunataka pia kuhamasisha uongezaji wa thamani katika zao hili la korosho, kwa hiyo lengo letu la kushiriki maonyesho hayo ni kuonyesha wadau na washiriki wa maonyesho hayo ya sabasaba kwamba zipo fursa nyingi za uongezaji wa thamani katika zao hili,”alisema Alfred.
“Cha kwanza ni katika kuongeza ubanguaji, sasa hivi tunabangua wastani wa asilimia 10 ya korosho zetu zote ambazo tunazizalisha , kwa hiyo tunataka kuongeza ubanguaji ufike asilimia 60 kufikia mwaka 2025/26, kwa hiyo hapa tunaonyesha wadau mbalimbali fursa zilizopo kwenye upande wa ubanguaji wa korosho , tuuze zaidi korosho iliyoanguliwa kuliko kuuza korosho ghafi na tukifanya hivyo tutakuwa na uhakika zaidi wa soko la korosho,”alisema Alfred.
Alisema kufanya hivyo kutaongeza uhakika zaidi wa soko la korosho kwa sababu wataweza kuuza katika nchi nyingi kuliko ilivyo sasa hivi ambapo wanategemea soko kutoka katika nchi mbili ambazo ni India na Vietnam.
Pia, alisema wanataka kupanua wigo wa soko kwa kubangua korosho na kuziuza katika nchi za Marekani, Bara la Ulaya, Mashariki ya Kati, China, Uarabuni, Bara la Afrika.
“Lakini pia tunataka kupanua soko la ndani, sasa kwa walaji wa soko korosho la hapa nchini ambalo bado ni dogo sana kwa sababu ya bei, lakini tukiongeza ubanguaji bei zitashuka na ulaji wa korosho nchini utaongezeka,”alisema Alfred.
Alisema Julai saba(7) mwaka huu watakuwa na siku maalum ya kuwagaiwa korosho bure washiriki wa maonyesho hayo na kwamba lengo likiwa ni kuhamasisha watu wale korosho ili wapate manufaa ya zao hilo.
“Tunataka zao la korosho liwe na manufaa zaidi katika jamii kwa maana kwamba na njia pekee ni wadau mbalimbali kushiriki katika mnyororo thamani wa zao hili kuanzia shambani na uongezaji wa thamani wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao hilo.
Kwa upande wake Domina Mkangara, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Udhibiti Ubora wa Bodi ya Korosho, alisema wameshiriki katika maonyesho hayo kuonyesha Watanzania fursa mbalimbali zilizopo katika zao hilo.
Mkangara alisema ni vema Watanzania kupendelea kura korosho kwa kuwa ina manufaa kubwa na kwamba zipo bidhaa mbalimbali watajioneza katika banda hilo ili kufahamu eneo la kuwekeza katika zao hilo.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa