Na Yusuph Digossi, TimesMajira Online
RAIS wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameshuhudia timu ya Yanga ikienda mapumziko ikiwa kifua mbele baada ya kupata goli la kuongoza lililofungwa dakika ya 12 na Zawadi Mauya.
Katika mchezo huo namba 208 wa kiporo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Rais Samia aliingia uwanjani dakika moja kabla timu hazijaingia uwanjani jambo lililoibua shwangwe kwa mashabiki waliojitokeza kushangilia timu zao.
Katika mchezo huo, Yanga walianza kwa kasi na kulishambulia lango la wapinzani wao na dakika ya 11 walipata kona iliyopigwa na Deus Kaseke na kisha kuokolewa na Aishi Manula lakini wapipata kona ya pili lakini wakiwa katika harakati za kuokoa Mauya alipiga mpira iliombabatiza Shomari Kapombe na kupoteza muelekeo wa Manula na kisha kuingia wavuni.
Goli hilo kwa namna fulani liliwazindua Simba ambao walipata kona ya kwanza dakika ya 14 lakini haikuweza kuzaa matunda na licha ya kujaribu mara kadhaa kupata goli la kusawazisha lakini mipango ya Yanga ilikuwa migumu.
Hadi wanakwenda mapumziko, Yanga walikuwa mbbele kwa umiliki wa mpira kwa asilimia 52 kwa 48 za Simba ambao walikuwa wamepiga mashuti matatu na moja pekee ndilo lililolenga lango dhidi ya mashuti sita ya Yanga ambayo matatu yalilenga lango.
More Stories
Watumishi wa Fahari wafanya Bonanza
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship