Na Mwandishi wetu,TimesMajira,Online
Mkuu wa Wilaya ya TemekeĀ Jokate Mwegelo ameweka wazi mbele ya waandishi wa habari dhamira yake ya kubadilisha taswira ya muonekano wa eneo la mbele la ofisi yake iliyopo uwanja wa Benjamin Mkapa Temeke, Dar es Salaam.
Akiongea katika eneo la tukio mapema leo Mkuu wa Wilaya amesema eneo hilo lina taswira ya Kitaifa na Kimataifa kwa kuwa hutumika katika michezo na dhifa mbalimbali.
Pia eneo hilo ndipo ilipo ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambalo nyakati za usiku huwa na giza linalopelekea vitendo vya kihalifu kufanyika.
“Mkuu wa Wilaya ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama haitaleta afya hata kidogo uhalifu kufanyika eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kwa Temeke usalama ni moja ya kipaumbele” AmesemaĀ Mwegelo.
Kwa upande wa Meneja wa TARURA ambaye pia ni mratibu wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam amesema kuwa zoezi hilo la ukarabati na uwekaji wa taa 32 katika eneo hilo la barabara lenye urefu wa kilometa 1.3 litagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 102 na litakamilika baada ya majuma mawili mara baada ya taratibu nyingine kukamilika.
Aidha Diwani wa kata ya Miburani Juma Mkenga amemshukuru Mkuu wa wilaya kwa kutambua umuhimu wa eneo hilo na kwamba uwekaji wa taa hizo kwa kiasi kikubwa utapunguza matukio ya uhalifu.
Eneo hilo kwa kipindi kirefu limekuwa likilalamikiwa na wananchi kwa kukithiri kwa vitendo vya kiuhalifu kama uporaji hasa nyakati za usiku.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Ā