November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkkuu wa mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akionyesha kitabu hicho.

Mtaka atoa rai kwa Waandishi wa vitabu

Na Zena Mohamed,TimesMajira Online Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amewataka waandishi wa vitabu nchini kuwapa mbinu waandishi wachanga kuhusu namna walivyofanikiwa ili kuwapa shauku na ari ya kujituma kwenye sekta hiyo.

Hayo yamesemwa jijini hapa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Mabala and the Internet cha Richard S.Mabala ambapo uliambatana na ufunguzi wa duka la vitabu la Elite Bookstore tawi la Dodoma.

Mkuu huyo wa mkoa amesema, wachapishaji wana mchango muhimu katika jamii hivyo ofisi yake iko tayari kuwapaushirikiano wowote wanaohitaji.

Pamoja na mambo mengine,Mtaka amesema,jamii inapaswa kubadilika na kujenga mazoea ya kutumia muda mwingi kujisomea vitabu ili kujifunza na kuwa na uelewa wa masuala mbalimbali.

“Vijana wengi hawana mazoea ya kusoma vitabu kutokana na uzembe,hali hii inawasababisha wengi kufeli kwenyemasomo hususan yanayohitaji tafiti (research),”amefafanua Mtaka.

Licha ya hayo Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma amesema, ili kufanikiwa zaidi kielimu,ni jukumu la wazazi na jamiikwa ujumla kujenga mazingira mazuri kwa watoto wao ambayo yatawapa nafasi na ari ya kusoma vitabu bila kusukumwa na mtu.

Mtaka alitumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha viongozi mbalimbali mkoani hapa kuona umuhimu wa kufanya kazikwa umakini na weledi mkubwa ili kukwepa mtego wa ‘balehe ya madaraka.

“Juzi nikiwa kwenye mkutano wa kuwaapisha ma DC niliwaambia kwamba hizi nafasi zisiwafanye viongozi wenzangu wakajisahau,kuna wengine wakipata nafasi kidogo wanabadili namba zao za simu,msijisahau mmeteuliwa kuwatumikia wananchi,”Mtaka amesisitiza.

Kutokana na umuhimu huo,taasisi inayojihusisha na Uchapishaji wa Vitabu nchini ya Africa Proper Education Network ilitoa jumla vitabu 4,190 vyenye thamani ya shilingi milioni 27 kwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuchangia jitihada zake katika kukuza elimu mkoani hapa.

Akikabidhi vitabu hivyo Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Hermes Damian ameeleza kuwa, ni wajibu wa wasoma vitabu kuendelea kuwaonesha wasisomaji faida nyingi zinazopatikana katika vitabu ili kuamsha ari na mwamko kusoma nakujifunza kupitia vitabu.

“Sisi Africa Proper Education Network hatuamini kuwa watu hawasomi kwakuwa hawapendi bali hawajashawishiwa kwa uoneshwa lulu zilizopo kwenye vitabu. Ni wajibu wetu kuwahamasisha,”amesema.