Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Mwanamitindo hapa nchini Hamisa Mobetto, ametoa shukrani za dhati kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba kwa kumteua kuwa Balozi wa kuhamasisha wananchi kulipa kodi.
Akitoa shukrani hizo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram, Mobetto amesema ni heshima kubwa sana kuteuliwa kuitumikia nchi yake hasa baada ya mamlaka husika kumuamini na kuona anafaaa.
“Nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uhai na hekima aliyoweka ndani yangu. Nimshukuru pia Rais wangu Mama Samia Suluhu Hassan na serikali nzima akiwemo Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba, kwa kuendelea kuamini vijana kwenye ujenzi wa Taifa letu.
“Kwa kutambua umuhimu wa kodi kwenye uendeshaji wa miradi ya nchi na kuchangia maendeleo ya Taifa, naahidi kuitumikia vyema nafasi yangu niliyoteuliwa ya ubalozi wa uhamasishaji wa ulipaji kodi kwa maslahi ya Taifa langu, naahidi kushirikiana na mabalozi wenzangu Edoku Mwembe na Mbwana Samatta pamoja na viongozi na wadau mbalimbali wa masuala ya ulipaji kodi!. Mwenyezi Mungu nisaidie,” amesema Mobetto.
More Stories
Mzee wa Bwax afunika ‘Kitaa food Fest’ Mbagala
TBL yazindua Kampeni ya ‘Smart Drinking’
Msimu wa nne,tuzo za eagle entertainment, kufanyika kivingine