Na Mwandishi Wetu,Timesmajira,Online
SERIKALI imehimiza uboreshaji wa mifumo mbalimbali ya usimamizi wa huduma za mawasiliano ili kuhakikisha kunakuwa na usalama na ubora wa huduma nchini.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea mifumo hiyo kwenye Taasisi ya Udhibiti katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam kati ya Juni 4 hadi 6, mwaka huu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amesema wananchi wanatarajia kupata huduma bora zenye usalama.
“Upatikanaji wa huduma bora za uhakika na salama ni jambo la msingi sana kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa” amesema Ndugulile.
Katika ziara hiyo, Ndugulile alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari na menejimenti alipotembelea mifumo ya udhibiti wa Mawasiliano.
Dkt. Ndugulile ameipongeza TCRA kwa ubunifu wa kujenga mifumo wezeshi kwa huduma mbalimbali za mawasiliano nchini, ambapo alisema uboreshaji wake ni muhimu sana.
Baadhi ya mifumo aliyotembelea na Waziri ni Mfumo wa Usimalizi na Udhibiti wa Masafa ya Redio na Televisheni na Kituo cha Kuratibu Majanga ya Kimtandao (TZ-CERT).
TZ-CERT pia itatoa ushuri wa kitaalam namna bora wa kudhibiti na kupambana ya majanga mbalimbali ya Kimtandao kwa Taasisi na makampuni mbalimbali hapa nchini.
Waziri pia ametembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja ambapo amehimiza TCRA kuendeza ushirikiano na Taasisi zingine zikiwemo za kiudhibiti kama Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa