Na Mwandishi Wetu,TimesMajira online,Dar
SERIKALI imehimiza uboreshaji wa Mifumo mbalimbali ya usimamizi wa huduma za Mawasiliano ili kuhakikisha kunakuwa na Usalama na Ubora wa Huduma Nchini.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea mifumo hiyo kwenye Taasisi ya Udhibiti, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam,Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Faustine Ndugulile (Mb) amesema Wananchi wanatarajia kupata huduma bora zenye usalama.
“Upatikanaji wa huduma Bora, za Uhakika na Salama nijambo la msingi sana kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi na Taifa” amesema Ndugulile.
Katika ziara hiyo Mhe. Ndugulile alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari na Menejimenti alipotembelea mifumo ya udhibiti wa Mawasiliano.

Dkt. Ndugulile aliipongeza TCRA kwa ubunifu wa kujenga Mifumo Wezeshi kwa huduma mbali-mbali za Mawasiliano Nchini, ambapo alisema uboreshaji wake nimuhimu sana.
Baadhi ya mifumo aliyotembelea Mhe. Waziri ni Mfumo wa Usimalizi na Udhibiti wa Masafa ya Redio na Televisheni na Kituo cha Kuratibu Majanga ya Kimtandao (TZ-CERT). TZ-CERT pia itatoa ushuri wa kitaalam-namna bora wa kudhibiti na kupambana ya majanga mbali-mbali ya Kimtandao kwa Taasisi na makampuni mbali-mbali hapa Nchini.
Waziri pia alitembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja ambapo alihimiza TCRA kuendeza kushirikiana na Taasisi zingine zikiwemo za Kiudhibiti kama Bank Kuu ya Tanzania (BOT).
More Stories
Kanisa la Shincheonji la Yesu nchini Ufaransa lakanusha ripoti ya Le Parisie
Vyombo vya ulinzi na usalama Mbeya,Benki kuu kushirikiana kutatua changamoto za utapeli mtandaoni
Polisi Mbeya kuimarisha ulinzi kuelekea sikukuu ya Pasaka