November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mo Noray asikitishwa mchezo wa Simba,Yanga kuahirishwa, amtaka Manji kurejea

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MDAU wa michezo na Shabiki mkubwa wa Yanga, ambaye pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi ya Tanzania Building Works L.T.D Mohamed Noray ‘Mo Noray’, amesikitishwa na kitendo cha Shirikisho la soka Tanzania (TFF), kuahirisha mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya Simba na Yanga uliokuwa ufanyike Mei 8 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Simba ndio walikuwa wenyeji, ambapo awali mchezo ulipangwa kufanyika majira ya saa 11 jioni lakini majira ya saa nane mchana kukatokea mabadiliko kutoka TFF kupitia Bodi ya Ligi kuwa mchezo huo umeahirishwa na kusogezwa mbele hadi saa moja usiku.

Kufuatia mabadiliko hayo, klabu ya Yanga haikuhafiki kucheza muda huo na walipomaliza program yao ya kupasha misuli moto majira ya saa 11 kasoro na kuwaona wapinzani wao kutotia timu na wao waliamua kuondoka na kutosikiriza amri ya TFF.

Akizungumza na TimesMajira Online mara baada ya mchezo huo kuahirishwa Mo Noray amesema, si jambo jema kuahirisha mchezo huo kutokana na ukubwa wa mechi za ‘Derby’ kama ilivyo Simba na Yanga hapa nchini kwani mashabiki mbalimbali walijitokeza kwa wingi kuhakikisha wanaushuhudia mchezo huo.

Mashabiki wengi wameumia akiwemo Mo Noray kwani wengine walitoka mbali nje ya Jiji la Dar es Salaam ili kuzishihudia timu zao zikitafuta pointi tatu muhimu ili kila mmoja ajiweke katika mazingira mazuri ya kunyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

“Ki ukweli niliumia sana, kwani walinikatisha furaha yangu ambayo nilitoka nayo tangu nyumbani hukizingatia nimekata tiketi halali lakini ghafra nasikia mechi imeahirishwa. Timu yangu imefanya maamuzi sahihi ili iwe fundisho kwa siku zijazo, kwani zipo timu huwa zinafanyiwa mchezo kama huu lakini zinashindwa kufanya maamuzi,” amesema Mo Noray.

Katika hatua nyingine Mo Noray amesema, licha ya klabu yao kupata ufadhili na GSM lakini anamtaka aliyekuwa mwenyewkiti wa klabu hiyo Yusufu Manji kurejea Yanga ili aongeze nguvu na mfadhili wa sasa kuhakikisha timu yao inafanya vizuri zaidi na kunyakuwa ubingwa msimu huu.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekaribisha wawekezaji hapa nchini, hivyo nivyema Yusufu Manji akarejea ili kuendeleza miradi yaake ambayo alikuwa amewaajiri watanzania wengi, naamini iwapo atarejea klabu Yanga itakuwa tishio katika mchezo wa soka hapa nchini,” ameongeza Mo Noray.

Amema, kipindi cha Manji aliiongoza klabu ya Yanga kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kutwaa ubingwa mara kadhaa, kwa kuondoa makundi katika klabu hiyo na kuwafanya wanachama, mashabiki na wapenzi kuwa kitu kimoja.