November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Real Madrid avikomalia vilabu 12 Ulaya

MADRID, Uhispania

RAIS wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez amesema, vilabu 12 ambavyo vilikubali kujiunga Ligi Kuu Barani Ulaya (ESL), vina mikataba ya kisheria na haviwezi kuondoka katika Ligi hiyo.

Takribani timu tisa kati ya 12, pamoja na vilabu vyote sita vya Ligi Kuu England, viliondoka kwenye mashindano yaliyopendekezwa Jumanne baada ya mpango huo kuzua taharuki kali huku Real Madrid, Barcelona na Juventus bado hawajaachana na mpango huo.

“Sihitaji kuelezea ni nini mikataba inavyofungamana, lakini kwa kweli vilabu haviwezi kuondoka. Baadhi yao, kwa sababu ya shinikizo, wamesema wanaondoka. Lakini mradi huu upo sawa kabisa, utasonga mbele na natumai hivi karibuni utafanikishwa,” Perez ameliambia gazeti AS.

Perez alisema, Alhamisi iliyopita baada ya Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham kujiondoa, kwamba ESL bado ipo tu. Klabu za La Liga Atletico Madrid na za Italia AC Milan na Inter Milan pia wamejitoa rasmi, wakati mwenyekiti wa Juventus, Andrea Agnelli alikiri mradi huo hauwezi kuendelea tena.

European Super League ya timu 12 ilitangazwa Jumapili na kupingwa vikali na tangu wakati huo imesababisha maandamano makubwa nje ya viwanja vya Timu zilizokubali kushiriki huko England.