November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yaagiza vifaa vya umeme kutengenezwa nchini

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Mtwara

WAZIRI wa Nishati Medard Kalemani amelitaka Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuhakikisha vifaa vya umeme vinatengenzwa hapa Tanzania ili kurahisisha na kuharakisha utengenezaji na marekebisho wa mitambo ya umeme pindi inapoharibika

Waziri Kalemani alitoa wito huo mwishoni mwa wiki liyopita wakati alifanya ziara mkoani hapa kwa ajili ya kufuatilia uharibifu wa mitambo na shughuli za ukarabati unaoendelea katika mtambo wa kuzalisha umeme kutumia gesi mkoani hapa.

“Ninatoa wito vifaa vyote vya umeme ‘spear parts’ vizalishwe hana nchini, nawaangiza ‘Plant Manager’ wote mahala ambapo mfumo wa kuzalisha umeme unatengenezwa lazima kuwepo na ‘spear parts’ hapo hapo ‘site’ na wala sio makao makuu ili mtambo unapoharibika wanfunga moja kwa moja,” amesema.

“Kuna manufaa yake ya kuwa na ‘spear parts’ karibu, jana kuna transfoma iliyofungwa hapa jana ilitoka gari mara moja ikarudi na tukaweka transfoma tusingekuwa tunazalisha hapa hizo transfoma tungepata wapi kwa jana hiyohiyo,” amesema.

Amelitaka shirika hilo pia wawaambie wanaotengeza vifaa vya umeme huko nje walete viwanda vyao hapa nchini ili kuzalishia hapa hapa kurahisha upatikanaji wa ‘spear parts haraka’.

Aidha alitoa siku mbili kwa watendaji hao, kuunganisha mitambo miwili mpya iliyofungwa kituoni hapo katika mfumo unaotumia teknolojia ya Kisasa kuendesha mitambo hiyo ili kubaini kwa haraka tatizo linapotokea, badala ya mfumo wa kizamani unatumika sasa.

Aidha amelitaka TANESCO wawe na utaratibu wa kufundishana na kupata mafunzo ya mara kwa mara juu ya ukarabati wa mitambo badala ya kutegemea wataalam kutoka nje ya nchi.

“TANESCO mna uzoefu wa miaka mingi katika kukarabati mitambo hii, rithishaneni utaalam, mkurugenzi awape mafunzo ya mara kwa mara, msitegemee watalaamu kutoka nje wanatuchelewesha, sababu ukimuhitaji leo kama anamambo yake hawezi kuja kwa wakati, najua uwezo huo mnao, amesisitiza Dkt. Kalemani.

Na katika kuboresha huduma ya upatikanaji wa umeme alitoa miezi mitatu kwa TANESCO kufungwa vifaa maalum katika njia za kusafirisha umeme nchi nzima, vinavyofanya kazi ya kidhibiti hitilafu ya umeme inapotokea isiathiri eneo jingine.

Vifaa hivyo huimarisha hali ya umeme na endapo hitilafu itatokea eneo A, haiwezi kuathiri eneo B, pia itarahisisha kubaini eneo la tatizo katika eneo lililoathirika pasipo kuzima umeme katika eneo lote.