November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TMDA: Tumepunguza dawa bandia/duni sokoni

Na  Aveline  Kitomary, TimesMajira Online, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Dawa,Vifaa tiba na Vitendanishi (TMDA) imefanikiwa kupunguza dawa duni na bandi sokoni kutokana  na ufuatilijia wa mara kwa mara na  uwepo wa mashine za kisasa.

Akizungumza  na wanahabari waliofanya ziara katika maabara iliyopo jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa TMDA, Adam Fimbo amesema kiwango cha dawa ambazo hazikidhi vigezo zinazotakiwa sokoni kwa sasa ni asilimia moja tu.

“WHO  inasema kwa nchi zote za Afrika dawa duni na bandia  ni asilimi 10 mwaka 2018, hakukuwa na  takwimu za kila nchi  lakini sisi tunapima kwa kuangalia kaguzi zetu sampuli tunazokusanya kupitia bidhaa tunazofuatilia kwenye soko ,huwa tunaanda taarifa za maabara kupitia chunguzi ndio tunapata takwimu tunaangali katika kipindi hiki tumechunguza sampuli kiasi hiki na tunalinganisha na dawa zilizosajiliwa sokoni ,”amebainisha Fimbo.

Amesema kupungua kwa dawa bandi kunatokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika  katika maabara za mamlaka hiyo.

“Tumewekeza katika maabara kwa vifaa mbalimbali za kisasa tumefundisha wataalam mbalimbali ili kubobea katika upimaji  dawa vifaa tiba na Kila miaka miwili tunashiriki kupimwa umahiri kwa wachunguzi wa maabara na ni sharti kuwa lazima tufanye ili tujue kama kweli wameiva.

“Tuna mashine nyingi za kisasa tumewekeza  karibu Sh bilioni 5 na zaidi kwa maabara ya Mwanza na Dar es Salaam ni uwekezaji mkubwa na mashine hizo zimekuwa msaada kufanya tunayoyatarajia,”ameeleza .

Fimbo amesema maabara inasaidia kufanya maamuzi ya kiudhibiti kwa dawa  kama kuanglia ubora na uwezo wa dawa kutibu.

“Ukiangalia kidoge huwezi kujua kwa macho kama kuna dawa na hata dawa ya maji huwezi kujua ndani yake kama kuna dawa au haijachafuliwa hivyo ni maabara tu ndio inafanya kujua kiwango cha kemikali kinachotakiwa na kama inasaidia  hivyo maabara ni kiungo muhimu katika kufanya shughuli za udhibiti.

“Tunakusanya sampuli maeneo tofauti  kama maeneo ya vituo vya forodha ,soko  ni lazima tupime kama viambata vilivyoko kwenye dawa vipo na hakuna uchafuzi na kama dawa inauwezo wa kufanya kazi inayotakiwa katika mwili wa mwanadamu.

“Na sio dawa tu  tunapima  na kondom sahivi unaweza kujua kama kuna matundu au la maabara inasaidia kuona hii inaondoa hatari kwa watumiajia na barakoa tunapima kuona kama kuna ubora unaopaswa,”amefafanua Fimbo.

Amesema mamlaka hiyo inamaabara hamishika 25 ili kufanya urahisi wa vipimo kwa maeneo ya mbali.

“Ukiwa na  maabara inayotimiza matakwa WHO  inakutangaza kupitia ukarasa wake  ,nchi zingine zinakuja kujifunza na tunapokea sampuli kuzipima  kama Lethoto ,Zambia,Malawi,Kenya ,Uganda  na nchi zingine wanakuja,”ameeleza Fimbo.