Na Penina Malundo,TimesMajira Online
MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Selemani Zedi, amesema Kamati ya LAAC imeteuliwa jana na Spika wa Bunge Job Ndugai yeye kuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo.

Amesema wajumbe wa kamati hiyo wameanza kupewa mafunzo ya wiki moja ya kuwajengea uwezo ili kuweze kusimamia matumizi ya rasilimali za umma zinazopelekwa kwenye Halmashauri zote 185 Tanzania.
Amesema kwa mujibu wa majukumu yao kikanuni,watahakikisha rasilimali za umma zinazopelekwa halmashauri zinatumika kama zilivyokusudiwa,na matumizi yote yanafanyika kwa mujibu wa sheria ya fedha ya Serikali za Mitaa.
More Stories
Kiongozi wa Mwenge awataka RUWASA kukamilisha mradi wa maji kwa wakati Kilindi
Balozi Nchimbi aongoza waombolezaji kumuaga Mzee Mongella
Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kumuua mama yake mzazi