November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mesut Ozil

Tetesi za soka Ulaya leo Jumanne 08.12.2020

Mesut Ozil

KIUNGO wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, mwenye umri wa miaka 32 raia wa Ujerumani ana uhakika wa asilimia 90, kujiunga na Fenerbahce mwezi ujao, kwa mujibu wa mmoja wa wajumbe wa bodi ya Fenerbahce .(Sport Digitale, via Mirror)

Wawakilishi wa Jesse Lingard wanapitia ofa za mkopo kwa kiungo huyo wa Manchester United na England mnamo Januari, na Real Sociedad moja ya vilabu ambavyo wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Sky Sports )

Frank Lampard

Kocha wa Chelsea Frank Lampard amesema hana shinikizo la kumuuza mlinda mlango wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, mwenye umri wa miaka 26, ambaye thamani yake pauni milioni 71,(Evening Standard)

Manchester United inaweza kumgeukia mlinzi wa pembeni wa Real Madrid ya Uhispania, Lucas Vazquez, mwenye umri wa miaka 29, wakati wanatafuta mshindani wa Mwingereza Aaron Wan-Bissaka, mwenye miaka 23.(Defensa Central – in Spanish)

Manchester United wana nia ya kumruhusu mlinda mlango wa Argentina Sergio Romero kuondoka mwezi ujao na watamuuza ikiwa dau la pauni milioni 2 litafikiwa.(Football Insider)

Mshambuliaji wa Brazili Hulk, mwenye umri wa miaka 34, ameondoka Shanghai SIPG na amehusishwa na taarifa za kuhamia ligi ya primia kwa uhamisho huru.(Sun)

Tottenham na Arsenal wanapigana vikumbo kumtaka kiungo wa kati wa AC Milan raia wa Ivory Coast, Franck Kessie mwenye umri wa miaka 23, ambaye ana thamani karibu pauni milioni 45 na ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika Juni 2022. (Calciomercato – kwa Kiitaliano)

Liverpool ina matumaini ya kuanza mazungumzo na kiungo mkabaji Faninho, 27, kuhusu mkataba mpya hivi karibuni.(Guardian)

Mholanzi Jetro Willems amekataa ofa ya mkataba mpya katika klabu ya Eintracht Frankfurt, hatua inayotoa fursa kwa Newcastle kumsajili mlinzi huyo, ambaye alikuwa akichezea Magpies kwa mkopo msimu uliopita. (Chronicle)

Newcastle wanalenga kurudi katika kambi yao ya Benton Jumanne huku wakitafuta kuendelea na mazoezi baada ya ugonjwa wa Covid-19 kusababisha kuahirishwa kwa mechi yao na Aston Villa. Magpies wanatumai mechi yao na West Brom itafanyika kama ilivyopangwa mwishoni mwa wiki hii.(Chronicle)