Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limefuta mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho kati ya timu ya Al Rabita ya Sudani Kusini dhidi ya Namungo FC iliyokuwa ichezwe leo kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
CAF imetangaza uamuzi huo baada ya Chama Cha Soka cha Sudani Kusini (SSFA) kushindwa kukamilisha taratibu kuhusu Waamuzi waliopangwa kuchezesha mechi hiyo.
Awali mchezo huo wa marudiano ulikuwa kuchezwa Sudani Kusini, lakini Al Rabita kupitia SSFA waliomba uchezwe Dar es Salaam kutokana na hali ya usalama nchini mwao kutokuwa shwari na ombi lililidhiwa na CAF.
Kabla ya mcheo huo kuahirishwa Namungo walipanga kuendeleza ubabe katika mchezo huo ambao licha ya kuwa wageni lakini bado walikua na faida ya kuendelea kuwa katika ardhi yao ya nyumbani
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Novemba 28, Namungo ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 3-0 na walikuwa hakiingia katika mchezo kusaka ushindi mwingine ili kutinga katika hatua ya pili ya mashindano hayo.
Kwa sasa timu hiyo inasubiri taarifa rasmi kutoka CAF kuona kama mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine au watatangazwa kusonga katika hatua ya pili na kukutana na El Hilal Obeid Kutoka Sudani ambapo mechi ya mkondo wa kwanza imepangwa kuchezwa Desemba 22 au 23 huku ile ya marudiano ikichezwa kati ya Januari 5 au 6, 2021.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025