October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Lionel Mess

Tetesi za Soka Ulaya leo Jumanne tarehe 03.11.2020

Lionel Mess

Klabu ya Manchester City huwenda ikampa ofa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, mwenye umri wa miaka33 raia wa Argentina, mkataba wa awali mwezi Januari kabla ya kuhamia England msimu ujao. (Daily Telegraph)

Mbali na hivyo, klabu hiyo pia inajiandaa kumfanya mshambuliaji wa England Raheem Sterling, mwenye umri wa miaka 25 na kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, mwenye umri wa miaka 29 kuwa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi katika Ligi Kuu England. (90 Min)

Atletico Madrid inapigana vikumbo dhidi ya Bayern Munich na Sevilla kumfuatilia kwa karibu beki wa kulia wa Brighton Tariq Lamptey, mwenye umri wa miaka 20. (Mail)

Nayo Man United, Leicester na Everton wamevutiwa na winga wa Kimatiafa wa Nigeria anayekipiga Villarreal Samuel Chukwueze, mwenye umri wa miaka 21. (90 Min)

Dele Alli

Klabu ya Paris St-Germain itakuwa makini katika uhamisho wa mchezaji wa England anayekipiga Tottenham Dele Alli, mwenye umri wa miaka 24, ikiwa atapatikana mwezi Januari. Klabu hiyo ya ufaransa ilifanya majaribio matatu yaliyogonga mwamba ya kumsajili kwa mkopo kiungo huyo wa kati msimu huu. (Mail)

Barcelona imeongeza nia yake ya kumnasa mshambuliaji wa Benfica raia Uruguay Darwin Nunez,21, kama mbadala wa muda mrefu wa Luis Suarez.

Barcelona itatoa ofa mpya ya pauni milioni 7 kwa mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Uhispania Eric Garcia mwezi Januari.

Mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 19 anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu, Barca ikipendelea kumsajili. (Mirror)

Kuacha kibarua cha urais wa Barcelona kwa Josep Maria Bartomeus kunaweza kufanya mpango wa uhamisho wa Garcia au mshambuliaji wa Lyon Mamphis Depay, mwenye umri wa miak 26 kuwa mgumu mwezi Januari. (Marca)

David Alaba, 28, ameikosoa Bayern Munich baada ya kugundua kuwa klabu imeondoa ofa yao ya mkataba mpya. Mkataba wa mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi utakwisha mwishoni mwa msimu huu. (Mail)

Paris St-Germain ilitaka kumsajili Thiagi Alcantara, mwenye umri wa miaka 29, msimu huu lakini badala yake iliishia kwa kaka yake Rafinha, mwenye umri wa miaka 27, baada ya kiungo huyo wa kati kuondoka Bayern Munich kwenda Livepool. (France Football)

Kocha wa Inter Milan Antonio Conte, 51 amesema alikacha mara mbili nafasi ya kuifundisha Real Madrid kwakuwa hakutaka kuchukua jukumu hilo kwa timu ambayo tayari ilishauanza msimu wake. (Marca)

Kocha mkuu wa Brighton Graham Potter amemuacha mfungaji bora Neal Maupay,24, katika mechi dhidi ya Tottenham siku ya Jumapili kwa kuwa mshambuliaji huyo ana tabia isiyopendeza (Daily Telegraph)