December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BREAKING: Magufuli ashinda tena Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Na Penina Malundo, TimesMajira Online, Dar es Ssalaam

TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imemtangaza Dkt. John Magufuli  ameshinda kuwa Rais wa Tanzania kwa kushinda  kura 12,516,252 huku akifuatiwa na Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Tundu Lissu akipata kura 1,933,271.

Mnamo Oktoba 28,2020 Watanzania waliungana kupiga kura  kwaajili ya kuwachagua viongozi mbalimbali ikiwemo nafasi ya Urais, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani kutoka sehemu mbalimbali ya nchi.

Akitangaza matokeo hayo leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere,Mwenyekiti wa NEC , Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema baada ya kukamilisha zoezi la kuhesabu kura  za uchaguzi mkuu  huo,mawakala wamepewa matokeo hayo kutoka majimbo 264 nchi nzima na tayari kusaini matokeo hayo.

Wengine ni Leopard Mahona (NRA) 80,787, John Shibuda (ADA TADEA) 33,086, Muttamwega Mgaywa (SAU) 14,922, Cecilia Mwanga (Demokrasia Makini)14,556 , Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi) 19,966 , Ibrahim Lipumba (CUF) 72,885, Philipo Fumbo (DP) 8,283, Bernard Membe (ACT-Wazalendo) 81,129 na  Queen Sendiga (ADC)7,627.

Wengine ni  Twalib Kadege (UPDP) 6,194 , Hashim Rungwe (CHAUMMA) 32,878,  Khalfan Mazrui (UMD) 3,721 na Seif Seif (AAFP) 4,635.