November 17, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TAPSHA na mkakati wa chakula shuleni

‎Na Israel Mwaisaka, Nkasi

‎UMOJA wa wakuu wa shule za msingi (TAPSHA) wilayani Nkasi mkoani Rukwa  umedhamiria  kuona suala la upatikanaji wa chakula shuleni kwa mwaka 2027 linafanikiwa kwa asilimia 100.

‎Akitoa taarifa ya utekezaji wa TAPSHA kwenye  mkutano mkuu wa mwaka 2026 Mwenyekiti wa umoja huo  Mulinga Joramu amessema suala la upatikanaji wa chakula shuleni limeonyesha mafanikio makubwa katika sekta ya elimu na kuwa jambo hilo limepewa kipaumbele katika kuona chakula shuleni kinapatikana katika shule zote za msingi wilayani Nkasi.

‎Katika Taarifa hiyo imeonyesha Wilaya Nkasi kufanya vizuri kwenye mtihani wa mwisho wa darasa la Saba kwa mwaka 2026 kimkoa na kuwa moja ya kitu kilichopelekea kuyafikia mafanikio hayo ni pamoja na upatikanaji wa chakula shuleni.

‎Alidaii kuwa licha ya mafanikio hayo waliyoyapata  mwaka huu lakini pia bado wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo uwingi wa Wanafunzi kwenye darasa moja,upungufu wa madawati,uhaba wa Walimu kwa baadhi ya shule,kukosekana kwa vifaa vya Tehama,uhaba wa nyumba za Walimu na zilizopo kutokarabatiwa,kutokuwepo kwa motisha kwa shule zinazofanya vizuri ikiwa ni pamoja na nyingine nyingi.


‎Akifungua mkutano huo Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Nkasi  Njogela  kwanza alipongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye matokeo ya darasa la Saba na kuwataka Walimu wakuu kupitia umoja wao huo kuendelea kusimamia taaluma shuleni ili waendelee kufanya vizuri kwenye mitihani ijayo.

‎Aliwataka Walimu hao kusimamia suala la upatikanaji wa chakula shuleni kama yalivyo malengo Yao na kuwa katika kufanikisha hilo Serikali ipo pamoja nao pale wanapopata changamoto yoyote katika kufanikisha mpango huo muhimu wa upatikanaji wa chakula shuleni.

‎Pia aliwataka Walimu wakuu hao kuhakikisha wanawasimamia  Walimu wanaowaongoza kuhakikisha wanajaza PEPMIS kwani hayo ni maisha yao kinyume  cha hapo watashindwa kupata haki zao za kimsingi ikiwemo upandaji wa madaraja na vyeo.

‎Alisema kuwa PEPMIS ndiyo kipimo  cha utendaji kwa watumishi wa Umma hivyo kitendo cha kupuizia ujazaji wa PEPMIS ni kujinyima haki hivyo ni muhimu kwa Walimu wakuu kuhakikisha Walimu wao wanajaza PEPMIS Kila wakati ili kuweza kuondoa malalamiko  kutoka kwao kwa kushindwa kupata haki zao zinazotokana na kutojaza PEPMIS.


‎Suala la uhaba wa madawati halmashauri imelipa uzito wa aina yake na kupelekea kutenga  Fedha kwa ajili ya mpango huo na kuwa wameweza kuzungumza na taasisi kadhaa za serikali ikiwemo TAWA na TFS kuweza kuwapatia kibali Cha kuvuna baadhi ya miti ambayo imedumu kwa muda mrefu ili waweze kupasua mbao zitakazotumika kutengenezea madawati kwa gharama nafuu.

‎Mkutano mkuu huo wa TAPSHA pia ulienda sambamba na uchaguzi baada ya waliokuwepo kumalizia muhula wao wa miaka mitano na waliochaguliwa ni  Alipo Jonas Jimmy Mwenyekiti,Wilson Mrisho Makamu Mwenyekiti, George Mkondya Katibu,Ezekia Kataupepo Katibu msaidizi na Teddy Mbaule Mhazina.


‎