Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online,Dar
IMEELEZWA kuwa umahiri wa utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) umewavutia wadhibiti wenza wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati, Maji, Mawasiliano na Usafiri(PURA) kutoka nchini Gambia, kuja hapa nchini kujifunza namna mamlaka hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa ufanisi na mafanikio.
Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Prof. Mark Mwandosya,Novemba 16,2026 akiwakaribisha wajumbe wa Bodi ya PURA ya Gambia,ameeleza kuwa EWURA huongozwa na misingi ya utendaji inayozingatia utaalam na uwazi.

Pia uhuru wa maamuzi ya kiudhibiti yanayozingatia maslahi ya watoa huduma, walaji na ya Serikali wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ili kuleta tija na matokeo chanya.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya PURA Gambia,Lucy Fye ameeleza kuwa, taasisi hiyo imevutiwa na umahiri wa EWURA katika mifumo yake ya kushughulikia malalamiko, utaratibu wa utoaji leseni na ufuatiliaji wa utendaji wa watoa huduma wanaodhibitiwa, mfumo wake wa utawala na uendeshaji pamoja na matumizi ya teknolojia ya kiwango cha juu katika utoaji wa leseni na vibali.


More Stories
Serikali yaendelea kuimarisha uratibu maandalizi AFCON 2027
Tanzania kuwakutanisha nchi za Afrika kujifunza Afya ya Mama na Mtoto
Wahimizwa kutumia soko la Uturuki kuuza mazao kilimo