November 9, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dakika 8 za Ndejembi zaibua matumaini kilimo cha bustani

Na Mwandishi Wetu, Timesmajiraonline

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameielekeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuongeza juhudi za kutafuta na kupanua masoko ya kimataifa kwa kubaini bidhaa zinazohitajika pamoja na viwango vya ubora vinavyotakiwa katika masoko hayo.

Amesema hatua hiyo itawasaidia wazalishaji nchini kuendana na mahitaji ya wanunuzi wa kimataifa, kuongeza ushindani wa bidhaa zao na kupanua mauzo nje ya nchi.

Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo wakati akitembelea mabanda ya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara na Uwekezaji wa Mazao ya Bustani, HortiLogistica Africa 2026, katika viwanja vya TGT mkoani Arusha, kabla ya ufunguzi rasmi.