
Na Mwandishi wetu, TimesmajiraOnline, Tanga.
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga, Philemon Magesa, amefanya kikao kazi na watendaji wa Kata na Mitaa, Maafisa afya na Tarafa kwa lengo la kuweka mikakati ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo huku akitaja vipaumbele vinne ambavyo ni ukusanyaji wa mapato, usafi wa mazingira, usimamizi wa miradi ya maendeleo na utawala bora na kutilia mkazo zaidi suala la ukusanyaji wa mapato kwa kuzingatia sheria.
Akizungumza katika kikao hicho, Novemba 6, 2026, Magesa amesema ukusanyaji wa mapato utafanyika kisayansi na kwa kuzingatia mifumo iliyowekwa huku akisisitiza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakao kiuka wajibu wa kulipa mapato ya Serikali ili kuongeza ufanisi na kudhibiti upotevu wa mapato ya Halmashauri
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Usafi wa Mazingira na Udhibiti Taka wa Jiji la Tanga Kizito Nkwabi amesema kupitia mfumo mzuri wa ukusanyaji wa mapato ya taka wataimarisha usimamizi wa magari ya taka ili kuhakikisha yanamudu kutoa huduma kwa jamii

Naye Mhandisi wa Jiji la Tanga Isaack Mpaki amesema watasimamia utoaji wa vibali vya ujenzi kwa kila anayejenga na kuweka alama kwa watakao kiuka taratibu za ujenzi kwa kujenga bila kibali ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.


More Stories
Chalamila kwenda Qatar kuishangilia Serengeti Boys
Rc.Chalamila atangaza rasmi mikakati ya kuboresha Dar
Watanzania milioni 25 kunufaika na bima ya afya kwa wote