Na Mwandishi Wetu,TimesMajira
UMOJA wa Ulaya (EU) umerudisha rasmi upatikanaji wa fedha za maendeleo za kiasi cha Euro milioni 156 (takribani Shilingi bilioni 461 za Tanzania) baada ya kuchelewesha kuidhinishwa kwa mpango huo kufuatia matukio ya Oktoba 29, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa ushirikiano wa Umoja wa Ulaya EU nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Marc Stalmans uamuzi huo ulifanywa tarehe 23 Julai, 2026 kwamba EU itaendelea na utoaji wa kiasi chote cha fedha hizo bila kupunguza bajeti wala kubadili upeo wa malengo ya shughuli zilizopangwa awali.
Umoja wa Ulaya mbali na kuwa mshirika mkubwa wa maendeleo wa Tanzania pia ni kinara wa ushirikiano wa maendeleo ya sekta za kilimo, nishati, miundombinu, biashara na teknolojia.
Takwimu za EU zinaonesha biashara baina ya pande hizi mbili ni euro bilioni 2.15 kwa mwaka 2025.

More Stories
Samizi:Uchunguzi wa mapema wa saratani ya matiti huokoa maisha
Tanzania,China zasaini makubaliano Elimu ya Ufundi
Serikali yaimarisha elimu Jumuishi,yatoa vifaa saidizi