Na Mwandishi Wetu,TimesMajira
BENKI ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Kanda ya ziwa imeendelea kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja yenye kaulimbiu ya The Extra Mile kwa kutembelea wateja wao.
Benki hiyo imetembelea wateja wanaojihusisha na uchakataji wa mafuta ya Pamba, viwanda vya kuchakata mpunga, ufugaji wa samaki , ujengaji wa maghara kwa ajili ya kuhifadhia mazao na vitendea kazi kama magari ya kubebea mazao.
Wengine waliotembelewa na benki hiyo ni Pamoja na wale wanaojihusisha na vifaa maalum vya kutunza baridi kwa ajili ya kihifadhi samaki, maziwa na nyama.
Taarifa ya TADB jana amesema Kanda ya Ziwa inaoongoza kwa kuwa na miradi mingi inayofikia bilion 300 na miradi inayoongoza ni Mpunga kwa kuwa na shilingi bilioni 118, ikifuatiwa na Kahawa kwa shilingi bilioni 88 pamoja na Pamba kwa zaidi ya shilingi bilioni 58
Amesema Kati ya shilingi bilioni zaidi ya 300 zinazotumiwa na benki katika kuchagiza miradi ya kilimo Kanda ya ziwa inapatiwa asilimia 33% ya mikopo yote kutokana na ukubwa wa eneo pamoja na miradi mikubwa ya kimkakati inayohusisha kahawa, mpunga, ufugaji kwa njia ya vizimba, ufugaji wa kuku na ng’ombe.

“Kanda ya ziwa itaendelea kuwa kinara katika utoaji wa huduma bora kwa wateja pamoja na kuendelea kuwa mfano bora wa kusimamia, kuzalisha na kuleta matokeo chanya kwa taifa letu na kwa pamoja tunasema kilimo kinabenkika”amesema taarifa ya benki hiyo.
Vishal Sodhia wa kampuni ya Vira 2018, alisema kabla ya uwezeshaji wa TADB walikuwa na mashine ya kawaida ya kukamua mafuta tani 150 kwa siku lakini baada ya uwezeshaji huo watakuwa na uwezo wa kukamua hadi tani 350 za mafuta ya mbegu za pamba kwa siku.
Emmanuel Masangwa wa Kampuni ya Masangwa Trading Company Ltd, amesema TADB imewawezesha kwenye ujenzi wa miundombinu ya kampuni yao na kuwaongezea uwezo wa kununua mazao.

“TADB kwa kweli wamekuwa msaada mkubwa kwetu kwa kutuwezesha na hata riba wanayotutoza ni ndogo sana pia tunaishukuru serikali kwa kuendelea kuiwezesha hii benki,” amesema Emmanuel
Naye John Saria wa Kampuni ya Sariake ameiishukuru Benkiy a TADB kwa kuamini maono yake na kuamua kumsaidia kwa kumpa mkopo ambao umesaidia kuinyanyua kampuni hiyo na kuongeza uzalishaji maradufu

More Stories
Transfoma nne zasafirishwa kwenda Mradi wa TAZA
Dkt Tulia: Mabunge yaweke nguvu kuboresha huduma za afya
EWURA yawakumbusha wateja haki zao