September 19, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ndejembi aungana na wananchi kufanya mazoezi.

Na Mwandishi Wetu.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, leo Septemba 19, 2026, ameungana na wananchi mbalimbali kufanya mazoezi katika barabara ya fukwe za Coco Beach kuelekea Daraja la Tanzanite, jijini Dar es Salaam.

Mazoezi hayo ni sehemu ya shughuli za kuhamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya na ustawi wa jamii.