MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei za mafuta, hali inayotarajiwa kuleta unafuu kwa watumiaji.
Kwa.mujibu wa taarifa ya EWURA kwa umma ,bei ya petroli imepungua kwa shilingi 102 kwa lita, huku bei ya dizeli ikishuka kwa shilingi 101 kwa lita.
Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha bei za mafuta nchini zinakuwa himilivu na kulinda maslahi ya wananchi, ikiwa ni pamoja na kuimarisha usimamizi wa soko na kuhakikisha upatikanaji wa mafuta kwa wakati katika maeneo mbalimbali nchini.
Hatua hizo zimechangia kupunguza athari za mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia.
EWURA imeonya kuwa wauzaji wa mafuta watakaokiuka bei elekezi watachukuliwa hatua kali za kisheria. Wakaguzi wa Mamlaka hiyo tayari wapo kazini katika maeneo mbalimbali kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa.
Aidha watumiaji wa mafuta wameshauriwa kuchukua risiti wanaponunua mafuta, kwani nyaraka hizo hutumika kama ushahidi kunapokuwa na changamoto yoyote.

More Stories
TANESCO yabaini matukio ya Wizi wa Umeme Kinondoni
DCEA yazindua klabu kupinga dawa za kulevya vyuoni
Ubunifu wa IFM wawavutia wananchi