Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online,Mwanza
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA)imendelea kusisitiza umuhimu wa uwajibikaji,ushirikiano na kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na endelevu za majisafi na usafi wa mazingira.
Ambapo Mkurugenzi wa MWAUWASA Mhandisi Mashaka Sitta,amewataka watumishi wa mamlaka hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na kujituma.

Huku akiwasisitiza watumishi hao kuzingatia utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kuhakikisha malengo ya mamlaka hiyo yanafikiwa.
Mha.Sitta amezungumza hayo Septemba Mosi,2026 wakati alipofanya kikao cha kawaida cha utendaji kazi na watumishi wa mamlaka hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa MWAUWASA jijini Mwanza.
Ambapo lengo la kikao hicho cha kila mwezi ni kukumbushana kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi, ikiwemo uwajibikaji,bidii,weledi na kuhakikisha kila mtumishi anatekeleza majukumu yake kwa ufanisi katika nafasi aliyopangiwa.
Mha.Sitta ametumia fursa hiyo kuwatambulisha viongozi wa vitengo mbalimbali vya MWAUWASA,na kupitia kikao hicho ulifanyika uchaguzi wa Baraza la Wafanyakazi, ambapo watumishi walipata fursa ya kuwachagua wenzake watakao wawakilisha katika baraza hilo.
Mara baada ya uchaguzi huo kukamilika Mha.Sitta amesema,ana imani waliochagiliwa kuwasilisha katika Baraza la Wafanyakazi katika kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kwa kuzingatia maslahi mapana ya watumishi na mamlaka kwa ujumla.
Aidha,amesisitiza umuhimu wa baraza hilo kuwa chombo chenye ushirikiano, mshikamano na mawasiliano mazuri, akiwataka wajumbe kufanya kazi kwa pamoja na kujenga mazingira mazuri ya ushirikiano kati ya watumishi na uongozi wa MWAUWASA.


More Stories
Ubunifu wa IFM wawavutia wananchi
Polisi wachunguza kifo cha mwanafunzi anayedaiwa kujirusha
Yas yatambulisha uzi mpya wa Zanzibar Marathon