Na Penina Malundo,Timesmajira
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa leo, Agosti 22, 2026, kuandika historia mpya nchini kwa kuzindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP), kilichopo Rufiji, Mkoa wa Pwani.
Uzinduzi huo unaweka alama muhimu katika safari ya Tanzania ya kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuongeza uzalishaji wa viwanda na shughuli nyingine za kiuchumi, huku ukitarajiwa kuchochea kasi ya maendeleo ya Taifa.

JNHPP ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati katika sekta ya nishati nchini, ikiwa na uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 za umeme. Kukamilika kwake kunatarajiwa kuongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme na kuimarisha upatikanaji wa nishati kwa wananchi na sekta mbalimbali za uchumi.
Kwa uzinduzi huo, Rais Samia anaweka historia nyingine katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kitaifa inayolenga kuimarisha miundombinu ya nishati na kuweka msingi wa uchumi unaotegemea uzalishaji wenye tija.



More Stories
Atlas yazalisha gesi kwa maji
Mbunifu wa dawa salama apunguza uharibifu wa mayai
Tulia Trust kuja kivingine,tamasha ngoma za asili