August 10, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DED Mkuranga atembelea maonesho ya nanenane Morogoro

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online,Morogoro

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Waziri  Kombo amewataka wawekezaji kujitokeza kuja kuwekeza katika wilaya hiyo ambayo ardhi yake haina migogoro

Kombo  ameyasema hayo mwishoni mww wiki alipohudhuria ufungaji wa maonesho ya Nanenane ya mwaka  2026 Kanda ya Mashariki katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Manispaa ya Morogoro

Amesema wawekezaji ambao wanataka kuwekeza katika wilaya hiyo wanatakiwa kufika katika ofisi za halmashauri hiyo zilizopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kupata baraka zote kwa viongozi.

Aidha, amesema katika bajeti mpya ya mwaka 2026/27 halmashauri imetenga maeneo mapya matano kwa ajili ya uwekezaji

” Tunawakaribisha wawekezaji wote kuja kuwekeza katika maeneo yaliyotengwa na halmashauri yetu kwa kufuata utaratibu uliowekwa na ili kuepuka migogoro,” amesema Kombo

Halmashauri ya Manispaa ya Mkuranga katika kuhakikisha kuwa wananchi pamoja na wadau wengine wa shughuli za Kilimo, Mifugo  na Uvuvi wanapata fursa ya kujifunza na kupata maarifa ili iwe chachu ya kuongeza tija katika uzalishaji imeendelea kuongeza kutenga maeneo ya uwekezaji,” amesema

Ameyataja maeneo mapya yaliyotengwa kwa uwekezaji katika bajeti mpya kuwa ni pamoja na Kazole, Kimanzichana, Mbezi,Nyamato na Msolwa.

Akizungumzia faida za kushiriki maonesho ya nanenane amesema  yamewawezesha kutangaza bidhaa zao sàmbamba na kutangaza mambo ambayo halmashauri inafanya

Awali wakati akikagua katika Banda la Halmashauri hiyo Kombo  amewasihi wajasiriamali kuhakikisha wanakuwa na nyenzo muhimu za kuhakikisha mbali na kuuza bidhaa zao lakini pia wanatumia jukwaa hilo kuwapatia uelewa wananchi.

Hata hivyo banda hilo pia lilitembelewa na madiwani wa Kata zote za Mkuranga na Wakuu wa Idara mbalimbali kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali na bidhaa zinazozalisha.

k