Na.Mwandishi wetu,Timesmajira.
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema utekelezaji wa hatua za mwisho za Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma utasababisha kukosekana kwa huduma ya umeme kwa muda katika baadhi ya mikoa, ili kupisha kazi za mkandarasi kwa usalama.
Hayo yamebainishwa mapema leo Julai 28,2026 Mkoani Pwani na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Irene Gowelle, wakati akizugumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mradi huo .
Amesema mradi huo umefikia asilimia 94 na unatarajiwa kukamilika Agosti 21, 2026 huku asisitiza Serikali kupitia TANESCO imefanya kazi kubwa katika utekelezaji wa mradi huo, ambao sasa umeingia katika hatua za mwisho.
“Hatua iliyobaki katika mradi ni sehemu ya maeneo ya Mkambalani, Morogoro na Kikombo, Dodoma, kazi inayohitaji kuzimwa baadhi ya njia za kusafirisha umeme”amesema Gowelle
Gowelle amesema kazi hiyo itafanyika kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza itaanza Julai 30 hadi Agosti 4, 2026 katika eneo la Mkambalani, Morogoro, awamu ya pili ikifanyika Agosti 11 hadi 17, 2026 katika eneo la Kikombo, Dodoma.

“Kutokana na hali hiyo kutakuwa na upungufu wa huduma ya umeme kwa baadhi ya wateja katika mikoa ya Kanda ya Kati, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Magharibi na Kanda ya Kusini Magharibi” amesema
Amesema kuwa hakutakuwa na kukosekana kwa umeme kwa siku sita mfululizo katika eneo moja, bali ratiba za katizo zitatofautiana kulingana na siku na maeneo yanayohusika.
Aidha amesema huduma hiyo itaaanza kukosekana kati ya saa 12:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni katika siku na maeneo tofauti huku akisisitiza kuwa si wateja wote watakosa umeme kwa siku zote za kipindi hicho.

“Ratiba za maeneo yatakayoathirika wananchi watapata kupitia vyombo vya habari, kupitia mitandao ya kijamii na matangazo rasmi ya WhatsApp ya TANESCO”amesema
Hata hivyo amesema mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara haitaathirika na zoezi hilo, huku mikoa mingine katika kanda ya kati, kaskazini, ziwa, magharibi na magharibi ikitarajiwa kuathirika kwa nyakati tofauti.
Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Chalinze kwenda Dodoma wenye urefu wa kilomita 345, Mhandisi Newton Mwakifwamba, amesema mradi huo una thamani ya takribani shilingi billioni 514 na umefadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali.
“Kukamilika kwa mradi huo kutasafirisha usafirishaji wa umeme wote unaotangaza katika Bwawa la Julius Nyerere wenye uwezo wa megawati 2,115, kufikia uhakika wa kufikia umeme nchini .
Aidha amewatoa hofu wananchi kwa kufafanua kuwa timu za wataalamu zimejipanga vyema kuhakikisha ujenzi huo hautaathiri kwa namna yoyote usafiri huo wa treni.

More Stories
Tanzania yaeleza hatua za ushirikiano uhifadhi Ngorongoro
Wizara ya maliasili na utalii yawasilisha rasimu ya miaka mitano
HGWT yaahidi kutekeleza mkakati wa kutokomeza ukeketaji