July 26, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Kikwete akutana na viongozi Chalinze wajadili Dira 2050

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Chalinze

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amekutana na kufanya mkutano na Madiwani na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, wakiwemo Watendaji Kata, Maafisa Tarafa, Wakuu wa Idara za Halmashauri ya Chalinze na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ramadhani Possy.

Kikao hicho kimetoa nafasi ya kujadili kwa pamoja majukumu na mipango ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 ambayo itawezesha Halmashauri ya Chalinze kutoa mchango wake mkubwa katika ustawi wa Taifa kwa kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa.