Na Mwandishi Wetu,Timesmajira
MECHI kati ya timu ya soka ya Chuo cha Future World na timu ya Chanika Veteran umemalizika kwa sare 1-1 huku ujumbe mkubwa katika mechi hiyo ni kuhamasisha vijana kujiunga na Chuo hicho kupata ujuzi.
Katika mechi hiyo iliyochezwa jana katika uwanja wa VODP uliopo Chanika kata ya zingiziwa wilayani Ilala jijini Dar es Salaam umeshuhudiwa na mamia ya wananchi wa Chanika na viunga vyake.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mechi hiyo Ofisa Masoko kutoka chuo Cha Future World Vocational David Msumba amesema lengo la mechi hiyo ni kukitambulisha chuo kwa wananchi hasa katika kata za Chanika na Zingiziwa

“Tumecheza mechi kati yetu Future World na Chanika Veterani na lengo kuu ni kuhamasisha wananchi kujiunga na chuo chetu ili kupata ujuzi kupitia kozi mbalimbali tunazitoa.”
Ametaja kozi zinazotolewa na chuo hicho ni ufundi wa magari na pikipiki, umeme wa majumbani,ulezi wa watoto wadogo,mafunzo ya urembo na ususi,Hotel Management pamoja na Computer Applications.
“Future World ni chuo chenye uzoefu wa karibu miaka 30 sasa, tangu kilipoanzishwa kwenye utoaji wa Mafunzo ya ufundi stadi katika fani mbalimbali.

“Hivi Karibuni, chuo hiki kimefungua tawi lake jipya eneo la Chanika kwa Ndevu eneo ambalo lina mandhari bora kabisa kwa utoaji wa elimu ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa hosteli nzuri za wanafunzi.
“Vijana hasa wahitimu wa kidato cha nne mnakaribishwa chuoni au kuingia kwenye Tovuti ya chuo na kupata fomu ya kujiunga na mafunzo uyapendayo”amesema Msumba


More Stories
Mawakili wa Serikali watakiwa kusimamia Utawala wa Sheria
0ryx Tanzania yazindua kitabu cha mwongozo Gesi ya LPG
NMB yatambuliwa Marekani kwa ubunifu wa bima kidijitali