Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
WANANCHI wa mtaa wa Nyamanoro Mashariki Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela mkoani Mwanza,wameendelea kuchukua hatua za kujenga barabara ya Sinza-Mjimwema yenye urefu wa takribani km 0.5 kwa kiwango cha zege.
Barabara hiyo ambayo inategemewa na wananchi zaidi ya 4,000 wa mtaa huo pamoja na mitaa ya Kata jirani ya Nyasaka.Huku Serikali na wadau mbalimbali wakiombwa kuunga mkono juhudi hizo ili barabara hiyo iweze kukamilika kwa haraka na ubora ili ipitike kwa urahisi wakati wote.

Akizungumza jana na Majira wakati wa zoezi la wananchi kufanya usafi na kupanga mawe eneo korofi la barabara hiyo ambayo ni hatua ya awali kabla ya kuanza zoezi la kumwaga zege, Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyamanoro Mashariki Missa Budundu,amesema moja ya jukumu la Mwenyekiti wa Mtaa ni kusimamia maendeleo kwenye mtaa wake.
Amesema zoezi hilo ni muendelezo wa utekekalezaji wa kujenga barabara ulioanza mwaka jan,hivyo katika kikao cha robo mwaka cha mtaa kilichofanyika hivi karibuni walikubaliana na wananchi kuwa kila kaya itachangia mfuko mmoja wa saruji ili kufanikisha ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha zege.
“Zoezi siyo kwamba linaanza ila ni muendelezo wa nyuma,tulisitisha baada ya mvua kuwa nyingi,hivyo tukasubili zipungue na sasa zoezi litakuwa endelevu na tumekubaliana kuwa kila Jumamosi tutakuwa turekebisha sehemu korofi wakati huo mchango wa saruji kwa kila kaya ukiwa unaendelea,”amesema Budundu.
Pia amesema,lengo ni kujenga barabara hiyo ili ikutane na barabara ya Mjimwema ni kiungo cha muhimu nkwa wakazi wa maeneo hayo kufika mjini kwa urahisi pamoja na maeneo mengine muhimu ikiwemo katika soko la ndizi na matunda Kiloleli.
“Tunazo sababu kwanini tunajenga hii barabara kwanza inaunganisha kwa upande wa chini kutokea barabara ya Greenview mpaka barabara kuu ya Makongoro-Airport,hivyo inawasaidia wananchi wa mtaa huu na wakata jirani ya Nyasaka kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa na hupataji wa huduma mbalimbali,”amesema Budundu.
Sanjari na hayo ameomba wadau mbalimbali kuwaunga mkono ili kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwani wananchi pekee hawaezi kwani ujenzi wake unahitaji fedha nyingi.
Kwa upande wake mmoja wa wananchi wa mtaa huo, Elizabeth Kalonga amesisitiza kuwa makubaliano yaliofanyika kupitia kikao cha robo cha mtaa huo ya kila kaya kuchangia mfuko mmoja wa saruji yasimamiwe na kila mmoja atimize makubaliano hayo.
“Mwenye nyumba akikisha tunashirikiana na wapangaji wako mnamchangia kiasi cha fedha kulingana na idadi yenu kisha mnanunua huo mfumo wa saruji Mpangaji atakayekataa mpele ofisi ya Serikali ya Mtaa akachukuliwe hatua kwani maendeleo ni ya wote na lazima kila mmoja hawajibike,”amesema Kalonga.
Naye Agnes Lucas,amesema kutegemea wananchi pekee si rahisi kukamilisha ujenzi hivyo aliomba waongezewe nguvu kutoka kwa Serikali na wadau mbalimbali,kwani anaamini barabara hiyo itafungua fursa zaidi za kiuchumi endapo itapitika wakati wote pamoja na kuimarisha wananchi kupata huduma muhimu kwa urahisi.


More Stories
Mwalimu VETA abuni vifaa kusaidia afya na elimu
Serikali yaendelee kuwawezesha mitaji vijana
Serikali yaweka mazingira rafiki kuvutia uwekezaji sekta ya elimu