
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar.
Vodacom yang’ara sabasaba, yatwaa tuzo mbili
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Daniel Chapo wakipokea maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Philip Besiimire, kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (SABASABA).
walipotembelea banda la Vodacom muda mfupi kabla ya ufunguzi rasmi wa maonesho hayo. Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Daniel Chapo Julai 3, 2026, katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo Vodacom Tanzania ilitunukiwa tuzo mbili, ikiwemo Tuzo ya Nafasi ya Tatu kwa Mshindi wa Jumla wa Maonesho yote na Tuzo ya Nafasi ya Pili ya Udhamini, ikiwa ni utambuzi wa mchango wake mkubwa kama mshirika muhimu wa Maonesho hayo.

Pichani ni baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (SABASABA), wakifurahia ushindi baada ya kampuni yao kutunukiwa tuzo mbili: Tuzo ya Nafasi ya Tatu kwa Mshindi wa Jumla wa Maonesho yote na Tuzo ya Nafasi ya Pili ya Udhamini, ikiwa ni utambuzi wa mchango wake mkubwa kama mshirika muhimu wa Maonesho hayo.

More Stories
WMA yazidi kuwafikishia elimu Wajasiriamali
TTB yamteua khalid al barwani kuwa Balozi wa Utalii
Serikali yaongeza kasi Mpango wa Umeme Nyuklia