Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeendelea kutangaza bidhaa na huduma za Tanzania katika soko la kimataifa kupitia ushiriki wake kwenye Kongamano la Kimataifa la Biashara na Uchumi la St. Petersburg (SPIEF 2026) nchini Urusi.
Ushiriki huo unalenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kuvutia masoko mapya kwa bidhaa za Tanzania chini ya kampeni ya Made in Tanzania.
Katika kongamano hilo, TanTrade imebainisha fursa kubwa zilizopo katika soko la Urusi kwa bidhaa mbalimbali za Tanzania zikiwemo kahawa, chai, karafuu, ngozi, korosho na mazao mengine yenye ushindani mkubwa kimataifa. Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi inayolenga kuongeza biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na mataifa mengine.

Aidha, TanTrade imewahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania kutumia fursa zinazojitokeza katika soko la Urusi na maeneo mengine duniani.
Kuimarika kwa usafiri wa anga kati ya Tanzania na Urusi kunatarajiwa kufungua ukurasa mpya wa biashara, utalii na uwekezaji, huku bidhaa za Tanzania zikizidi kupata nafasi katika masoko ya kimataifa ambapo kwa kuanzia tayari wadau wameanza kuwasilisha mahitaji ya bidhaa za vyakula Kahawa (green Coffee,), matunda ya parachichi, embe, papai na passion.
Aidha, shirika la Ndege ATCL linatarajiwa kuanza safari za Dar- Zanzibar- Moscow Mwezi Julai 2026 jambo ambalo litarahisisha usafiri wa wafanyabiashara.


More Stories
TBS kuadhimisha miaka 50,kuzindua kitabu chake
Vijana wahimizwa kutumia fursa za kiuchumi
DCP Ngoso, DCF Ngenya na DCI Mwaifuge wajionea huduma Magerezani