Na Mwandishi Wetu,TimesmajiraOline
BALOZI Mobhare Matinyi amewasili jijini Algiers, Jumanne, tarehe 19 Mei, 2026, tayari kuanza majukumu ya kuiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria.
Balozi Matinyi alilakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houri Boumediene na Mwenyekiti wa Mabalozi wa nchi wanachama za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) waliopo Algeria, Balozi Ndumiso Ndima Ntshinga wa Afrika Kusini; Balozi Toko Diakenga Serão wa Angola na Balozi Abdellatif Al-Layeh wa Misri pamoja na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania wakiongozwa na Kaimu Balozi Suleiman Mussa Rashid.
Balozi Matinyi aliteuliwa na kutangazwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 24 Aprili, 2026, kuwa Balozi wa Tanzania nchini Algeria baada ya kuitumikia nafasi hiyo jijini Stockholm katika Ufalme wa Sweden tangu Mei 2025.
Mbali ya Algeria, Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers huiwakilisha Tanzania pia katika nchi za Tunisia, Niger, Mauritania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi.




More Stories
CRDB Foundation,Zuchu wazindua jukwaa la “Zuchu – IMBEJU Masterclass
Hatifungani ya kwanza yazinduliwa iTrust
Ofisi ya Msajili wa Hazina yafanya mazungumzo na Balozi wa China